Tovuti za Serikali zadukuliwa nchini Kenya, wananchi wakosa huduma

November 17, 2025 1:12 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya maandishi yanayosomeka katika tovuti hizo ni pamoja na, ‘Access denied by PCP,, ‘We will rise again’, ‘White power worldwide’, na ‘14:88 Heil Hitler’.

Dar es Salaam. Tovuti za wizara muhimu za Serikali ya Kenya, ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani, Afya, Elimu, Nishati, Kazi na Maji, zimeathiriwa na shambulio la mtandao, jambo linalosababisha wananchi kutopata baadhi ya huduma na  usumbufu wa utendaji wa sekta hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini Kenya ikiwemo citizen, wananchi wengi wamekosa huduma kupitia tovuti hizo mapema asubuhi ya leo Novemba 17, 2025 baada ya wadukuzi kubadili muonekano wa kurasa za mtandao na kuondoa taarifa halali, kisha kuweka maandishi yasiyoidhinishwa. 

Baadhi ya maandishi yanayosomeka katika tovuti hizo ni pamoja na, ‘Access denied by PCP,, ‘We will rise again’, ‘White power worldwide’, na ‘14:88 Heil Hitler’.

Hadi sasa, mamlaka za serikali hazijatoa tamko lolote rasmi kuhusiana na shambulio hilo.

Shambulio hili linakumbusha tukio kama hilo lililotokea nchini Tanzania, ambapo baadhi ya akaunti za taasisi za Serikali zilikumbwa na shambulio la mtandao huku miongoni mwa akaunti zilizoathirika ni pamoja na akaunti ya mtandao wa X (zamani Twitter) wa Jeshi la Polisi pamoja na akaunti ya mtandao wa Youtube ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks