Mwili wa Mtanzania Joshua Mollel wawasili Tanzania, kuzikwa Novemba 20

November 19, 2025 5:52 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Viongozi wa Serikali wajitokeza kuupokea mwili wake uwanja wa ndege.
  • Atazikwa Novemba 20, 2025 Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.

Dar es Salaam. Mwili wa Mtanzania Joshua Loitu Mollel aliyefariki katika mapigano kati ya Israeli na Palestina wawasili nchini Tanzania ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu kutangazwa kwa kifo chake.

Leo Novemba 19, 2025 saa nane mchana mwili huo umewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka Tel Aviv, Israel na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Viongozi hao ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa,  Balozi Silima Haji Kombo na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandala 

Mollel anarudi kama mwenda zake baada ya ndoto alizokuwanazo kukatishwa ghafla na shambulio la Hamas lililofanyika nchini Israel mnamo Oktoba 7, 2023. Picha | MOF

Kuwasili kwa mwili huo nchini Tanzania ni matokeo ya makabidhiano yaliyofanyika kati ya Israel na Hamas, ambapo kabla ya kusafirishwa Ubalozi wa Tanzania nchini Israel jana (Jumanne, Novemba 18, 2025) ulifanya  ibada maalum ya kumuaga.

Kijana huyo wa kitanzania anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho Novemba 20, 2025, katika Mtaa wa Njiro, Kata Orkesumet, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.

Ndoto zilizokatishwa: Kutoka mafunzo ya kilimo hadi kifo kisichotarajiwa

Joshua Loitu Mollel (21) ni kijana wa Kitanzania aliyekuwa akifanya mafunzo ya kilimo huko Kibbutz Nahal Oz, kusini mwa Israel baada ya kuwasili nchini humo mnamo Septemba 2023 kupitia programu ya mafunzo ya kilimo mara baada ya kumaliza diploma yake ya masomo ya kilimo nchini Tanzania.

Mollel aliondoka Tanzania kama kijana mwenye ndoto na kiu za kutimiza malengo yake kupitia kilimo, lakini leo anarudi kama mwenda zake baada ya ndoto alizokuwanazo kukatishwa ghafla na shambulio la Hamas lililofanyika nchini Israel mnamo Oktoba 7, 2023, ambapo licha ya kufanya shambulio, Hamas waliteka watu hai na waliokufa zaidi ya 200, Mollel akiwa mmoja wapo. 

Juhudi za ufuatiliaji na uchunguzi kupata taarifa zake, zilifanyika kwa Serikali ya Israel na Tanzania mpaka pale Jeshi la Israel (IDF) lilipothibitisha kifo chake mnamo Disemba 13, 2023 na taarifa kutolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania. 

Joshua Mollel anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho Novemba 20, 2025, katika Mtaa wa Njiro, Kata Orkesumet, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara. Picha | MOF

Hata mara baada ya taarifa za kifo cha Mollel kufahamika, bado familia, ndugu jamaa na marafiki waliishi tu wakijua kuwa mpendwa wao amepoteza maisha, lakini hawakuwa na matumaini yeyote ya kumpokea, kumzika, au kumpa heshima anayostahili kutokanana mwili wake kuendelea kushikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza. 

Matumaini ya kurejeshwa kwa mwili wa Mollel yalianza kuonekana mara baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na wadhibiti wa kimataifa kufanyika na Hamas kukubali kurejesha miili ya mateka 22 waliokufa, miongoni mwao ukiwa mwili wa Joshua Mollel ambao familia na Watanzania waliokuwa wanaomboleza kifo chake kwa muda mrefu, wameupokea leo ili kuupumzisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks