Thamani ya shilingi imeimarika, utakatishaji fedha umedhibitiwa- Dk Mpango

April 1, 2019 11:28 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema mafanikio hayo yamepatikana katika kipindi kifupi cha utekekelezaji wa zoezi la ukaguzi na udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha kigeni.
  • Zoezi hilo lilitekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha ambapo baadhi ya maduka yalifungwa.
  • Huduma za ubadilishaji fedha za kigeni inapatikana katika benki za biashara na Shirika la Posta Tanzania

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la ukaguzi na udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni,  thamani ya shilingi ya Tanzania imeimarika huku matukio ya utakatishaji fedha yakidhibitiwa.

Zoezi la ukaguzi wa maduka ya ubadilishaji fedha za kigeni lilifanyika hivi karibuni katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha ambapo lilizua mjadala katika jamii kutokana na baadhi ya maduka yaliyokua yakifanya biashara hiyo kufungwa kwa kile kinachodaiwa kukosa leseni, kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa fedha haramu. 

Dk Mpango aliyekuwa akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa zoezi hilo kwa Wanahabari Jijini Dodoma leo (Aprili 1, 2019) amesema kutokana na kazi hiyo iliyofanywa na maafisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamefanikiwa kudhibiti matukio ya utakatishaji fedha haramu, jambo lililosaidia thamani ya shilingi  kuimarika.

“Katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la kudhibiti biashara ya kubadilisha fedha za kigeni thamani ya shilingi imeimarika na upatikanaji wa fedha za kigeni katika benki za biashara umekuwa mzuri,” amesema  Dk Mpango.

Amesema kabla ya kudhibiti biashara ya kubadilisha fedha za kigeni, Dola moja ya Marekani ilikuwa inauzwa kwa wastani wa Sh2,450 na baada ya utekelezaji wa zoezi hilo hivi sasa Dola ya Marekani inauzwa kwa wastani wa Sh2,300. 

Kutokana na zoezi hilo baadhi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yamefungwa kwa sababu ya kukiuka kanuni za biashara ambapo benki za biashara na Shirika la Posta Tanzania (TPC) zimepewa fursa ya kubalisha fedha za kigeni.

“Aidha benki za biashara kwa wastani  hivi sasa zinakusanya jumla ya Dola za Marekani 15 milioni kwa siku,” amesema Dk Mpango na kuongeza kuwa hali hiyo imesadia kuimarisha utendaji wa benki za biashara nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Isdor Mpango akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu na Kamishna wa Sera wa Wizara hiyo Mgonya Benedicto. Picha|Waziri wa Fedha na Mipango. 

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Mipango amesema Serikali imeandaa kanuni mpya za maduka ya ubadilishaji fedha za kigeni, zitakazoelekeza jinsi ya kuomba leseni za uendeshaji na masharti ya kuzingatiwa.

Kanuni hizo zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biashara hiyo ambayo hayataathiri sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla. 

Hata hivyo, imeelezwa kuwa lengo la ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni sio kufuta biashara ya maduka hayo bali ni kudhibiti ukiukwaji wa sheria uliokithiri na utakasishaji wa fedha haramu.


Soma zaidi:


Kwa upande wake, Gavana wa BoT  Profesa Florens Luoga amesema katika maduka 87 ya kubadilishia fedha za kigeni yaliyokaguliwa jijini Dar es salam maduka 82 yamekutwa na viashiria vya utakatishaji wa fedha.

“Kwa mfano maduka yaligundulika kutumia fedha nyingi za Tanzania kununua fedha za kigeni lakini fedha ndogo za kigeni hazikuwa na taarifa ya fedha za kigeni iliyobaki,” amesema Profesa Luoga. 

Amesema katika zoezi la ukaguzi hakuna fedha yoyote iliyotaifishwa na kuwa taratibu za ukaguzi zilifuatwa wakati wa kuchukua vielelezo mbalimbali zikiwemo fedha, simu za mkononi, kompyuta, mashine za kuhifadhia taarifa ili kusaidia uchunguzi. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV