Fahamu teknolojia inavyoweza kukusaidia kuamka mapema

March 9, 2023 8:53 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kupitia programu za kufuatilia muda unaopaswa kulala pamoja na mwenendo wa usingizi. 
  • Unaweza kuzitumia kukukumbusha muda wa kulala na kukuamsha muda wa kuamka.

Dar es Salaam. Kuwahi kuamka ni ndoto ambayo watu wengi huiota. Shughuli zetu za kila siku za kujitafutia kipato wakati fulani hututaka kuamka mapema.

Inawezekana wewe ni miongoni mwa watu waliowahi kukosa fursa, kushindwa kukamilisha jambo fulani kwa wakati na pengine kukumbana na adhabu kutokana na kuchelewa kuamka.

Kama haitoshi huenda umekuwa mtu wa kujiwekea nadhiri kila siku kuwa kesho nitaamka mapema huku ukitegesha alam lakini haiwi hivyo, basi usijari. Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia vitu vingi vimerahisishwa ikiwemo suala la kuwahi kuamka.

Makala haya yanaangazia namna teknolojia inavyoweza kukusaidia kuamka mapema ambapo ni kwa mujibu wa tovuti inayochapisha habari za  teknolojia ya nchini Marekani ya The Verge.


Soma zaidi


1. Tambua muda unaotumia kulala

Ili uweze kuamka mapema kwanza unapaswa kufahamu mwili wako unahitaji saa ngapi kupumzika. Kadri mwili unavyopata muda wa kutosha wa kupumzika ndivyo inakuwa rahisi kwako kuamka mapema.

Mahitaji ya mwili kupumzika hutofautiana kati ya umri na umri. Taasisi inayojihusisha na masuala ya usingizi ya Sleep Foundation ya nchini Marekani wanashauri mtu mwenye umri wa miaka 18 anapaswa kupata muda wa kuanzia saa saba za kulala.

Njia rahisi ya kufuatilia muda unaotumia kulala ni kupitia programu tumishi ambapo utazitumia kwenye simu au saa janja, unaweza pia kununua kifaa maalum kwa ajili ya kufuatilia muda unaopaswa kulala kama uchumi unaruhusu.

Programu tumishi zinazopendekezwa na The Verge ni pamoja na  Rise Science, Mintal Tracker, pamoja na Sleep Cycle ambazo hufanya kazi ya kukokotoa muda uliotumia kulala, muda unaopaswa kulala na mienendo yako wakati umelala.

Hata hivyo utalazimika kulipia kiasi kisichopungua Dola za Marekani 60 sawa na Sh140,000 za Tanzania kwa baadhi ya programu.

Saa janja (smart watch) ni miongoni mwa viwaa ambavyo huwa na programu maalumu za kufatilia muda unaotumia kulala. PichalNospeelessnight

2.Tumia vifaa janja kutengeneza ratiba ya kulala na mazingira rafiki kwa usingizi

Kuamka mapema kunategemeana na muda uliolala pia, kwa kutumia programu tumishi unaweza kuweka ratiba ya kulala na kuamka ambapo vifaa hivi vitakuwa na kazi ya kukukumbusha pale muda wa kulala unapokuwa umefika.

Wakati fulani si rahisi kuacha simu ukiwa unaperuzi, baadhi ya kampuni zimekuja na suluhu kwenye baadhi ya simu ambapo  unaweza ukaweka (bed time mode) ambayo hutumia akili bandia kubaini na kuzuia programu zote ambazo hukufanya uchelewe kulala.

Unaweza pia kununua taa maalumu ambazo ukifika muda wa kulala kujififisha mwanga wake ili kukupa nafasi ya kulala usingizi mororo. Baadhi ya taa hizi pia huwekewa uwezo wa kupiga alarm pale muda wa kuamka unapokuwa umefika.

Pamoja na teknolojia kurahisisha suala la kuwahi kuamka, bado kama huna nia itakuwa ni sawa na kazi bure.

Weka kwanza  nia ya kuamka mapema kwa kuzingatia ratiba zako za kila siku kisha teknolojia ije kukusaidia baadaye. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW