Tasac:Uchunguzi wa meli iliyozama Mwanza bado unaendelea

May 28, 2024 4:55 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema tayari imeanza kupokea taarifa za awali kuhusiana na ajali hiyo na uzembe wowote ukibainkka hatua zitachukuliwa.

Mwanza. Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ajali ya meli ya Mv. Claries iliyozama Mei 19, 2024 mwaka huu na iwapo kutabainika uzembe hatua zitachukuliwa.

Mkurugenzi wa Tasac, Mohamed Salum aliyekuwa akizungumza katika kikao kilichokutanisha wadau wa masuala ya usafirishaji wa meli Ziwa Victoria leo Mei 28, 2024, amesema wameshapokea taarifa ya awali kuhusiana na kuzama kwa chombo hicho na tayari wameshaanza kuchukua hatua za kiusalama kuzuia kutokea tena kwa ajali hiyo.

“Kila kukicha tunaendelea kujifunza kuhusiana na matukio yanayotokea kwenye vyombo vya usafiri majini, yapo matukio ambayo yametokea nchini ikiwemo ajali ya mv Bukoba na hata hii ya Mv Claries kama Tasac tutaangalia namna ya kufanya ili kuhakikisha usalama unakuwepo,” amesema Salum.

Taarifa ya Tasac inakuja zikiwa zimepita siku 9 tangu meli hiyo izame katika Ziwa Victoria ambapo bado shughuli ya kuitoa meli hiyo majini inaendelea.

Katika hatua nyingine, Salum amesema  kutoka na changamoto hiyo ipo haja ya kuwekeza katika masuala ya uokozi wa vyombo vya majini ili kusaidia pale inapotokea ajali ya ziwa au Bahari.

Naye Afisa Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL)ameishauri Serikali kuunda Kamati huru itakayosimamia uokoaji pale meli itakapopata changamoto baharini huku akiwatoa hofu wananchi juu ya matumizi ya usafiri huo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV