Tanzania yaanika afua 10 kudhibiti Ebola 

May 19, 2026 5:03 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa tetesi katika jamii na uchunguzi wa afya kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia mipaka, bandari na viwanja vya ndege.
  • Wizara ya Afya yathibitisha hakuna mgonjwa wa Ebola Tanzania.

Arusha. Serikali imewatahadharisha Watanzaniajuu ya uwepo wa ugonjwa wa Ebola ikitangaza afua 10 muhimu zitakazotumika kudhibiti ugonjwa huo ulioripotiwa katika nchi jirani za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Wizara ya Afya imetangaza afua hizo ikiwa ni takribani siku nne tangu nchi hizo zinazopakana na Tanzania ziripoti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na kutangazwa rasmi kuwa dharula ya kiafya ya kimataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Taarifa ya Mganga Mkuu wa Serikali Grace Maghembe, iliyotolewa jana Mei 18, 2026 inabainnisha kuuwa afua hizo zimetangazwa kutokana na ukaribu uliopo kati ya Tanzania na nchi zilizoripoti ugonjwa huo huku kukiwa hakuna kisa cha ugonjwa huo kilichoripotiwa hadi sasa.

“Kutokana na ukaribu na mwingiliano wa shughuli za kiuchumi na kijamii uliopo kati yetu na nchi zenye mlipuko huo, Serikali imeendela kuimarisha utayari na kuzuia ugonjwa huu kupitia afua mbalimbali,” imesema taarifa ya Maghembe.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya afua hizo ni pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa tetesi katika jamii na uchunguzi wa afya kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia mipaka, bandari na viwanja vya ndege ili kubaini mapema viashiria vya ugonjwa.

Nyingine ni kuimarisha utayari wa vituo vya huduma na kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa kinga na tiba muhimu ili kutoa huduma kwa wagonjwa endapo utaingia nchini pamoja na kupeleka timu za wataalam wa kitaifa katika mikoa yenye hatari kubwa ili kuimarisha hatua za kinga, ufuatiliaji na utayari wa kukabiliana ugonjwa huo.

Seikali pia imesema itaendelea kutoa elimu ya afya kwa umma kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo televisheni, redio na mitandao ya kijamii, kuimarisha ushirikiano na nchi jirani kupitia uratibu wa afya mipakani na ubadilishanaji wa taarifa za tahadhari na kutuma timu ya ngazi ya taifa katika mikoa iliyo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo.

Aidha, Wizara hiyo itatoa maelekezo kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na kuamsha timu za wataalam pamoja na kubainisha vituo maalum vya kuhudumia wagonjwa endapo kutatokea maambukizi

Kuendelea na vikao vya uratibu wa kitaifa kwa kushirikiana na Wizara za kisekta na wadau mbalimbali ili kuimarisha hatua za kuzuia Ebola  na kusambaza miongozo na vitendea kazi kwa mikoa na kuwakumbusha kuviweka katika hali ya kutumika endapo vitahitajika.

“Kuhuisha mwongozo wa wasafiri Travel Advisory) ili kutumika kuanzia tarehe 19 Mei 2026, kutekeleza afua za kinga kwa mujibu wa Kanuni za Afya za Kimataifa,” imeongeza taarifa hiyo ikirejea hatua ya 10 ya kudhibiti Ebola.

Pamoja na hayo, wizara hiyo imewataka watanzania kuchukua tahadhari zote za kiafya zinazohitajika ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kugusa maji maji ya mtu mwenye dalili za Ebola.

Ikiwa jamii itamshuku yoyote kuwa na dalili za ugonjwa huo Wizara ya Afya imewataka kutoa taarifa kupitia simu bila malipo kwa namba 199.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV