Tanzania, Hungary zafungua ukurasa mpya wa ushirikiano

July 18, 2023 12:54 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na ushirikiano wa biashara na uwekezaji
  • Sekta ya elimu kuimarishwa zaidi baina ya nchi hizo

Dar es Salaam.Tanzania na Hungary zimefungua ukurasa mpya wa uhusiano na ushirikiano wa kimataifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu na biashara.

Tangu mwaka 1980 nchi hizo zimekuwa na ushirikiano katika nyanja za diplomasia, uchumi, pamoja na biashara.

Ushirikiano huo licha ya kusuasua mwanzoni mwa miaka ya 1990 sasa  unategemewa kuimarika zaidi baada ya ziara ya Rais wa Hungary Katalin Novák.

Sekta ya uchumi kutazamwa upya

Rais Samia aliyekuwa akizungumza na wanahabari mara baada ya mapokezi ya Rais huyo leo Julai 18, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam, amesema bado kuna nafasi kwa nchi hizo kuimarisha zaidi ushirikiano katika nyanja ya biashara na uwekezaji ambao haukuwa vizuri miaka iliyopita.

“Tumegundua kiasi kidogo cha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Hungary na Tanzania ambao kwa mwaka 2022 ilikuwa Sh10.2 biilioni…kuna nafasi ya kuboresha na kuongeza,” amesema Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza jambo na Rais wa Hungary Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika maeneo mengine ya biashara Rais Samia na Rais Katalin  wamekubaliana kuhamasisha wawekezaji wa Hungary kuwekeza kwenye maeneo ya kimkakati yaliyopo nchini ikiwemo utalii.

Rais Samia amesema kwa miaka mingi tangu nchi hizo zianze uhusiano zimekuwa zikishirikiana katika utalii, mathalani mwaka 2022 ambapo Tanzania ilipokea watalii 7,188 kutoka Hungary.

“Tunaamini baada ya ziara yako watalii wengi watatembelea Tanzania, tunaalika wawekezaji kutoka Hungary kutazama fursa za uwekezaji katika utalii,” Ameongea Rais.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa kuhusishwa kwenye uwekezaji ni pamoja na utoaji wa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano, uvuvi uchimbaji madini, uzalishaji na fedha.

Aidha, Rais Samia na Katarin wamekubaliana kuweka uwezeshaji wa wanawake, maendeleo ya jinsia na watoto kama jambo la  kipaumbele katika mataifa yao.


Soma zaidi


Elimu kuimarishwa zaidi

Kwa upande wake Rais wa Hungary Katalin Novák aliye ziarani nchini Tanzania, amewaambia wanahabari kuwa suala la elimu ni moja ya kipaumbele baina ya nchi hizo na Serikali zote zitaendelea kutoa udhamini wa masomo kwenye nchi zao.

“Kuanzia leo kuna wanafunzi wengine kutoka Hungary wataanza kusoma nchini Tanzania kwa fedha za Tanzania nao wajifunze lugha na elimu yoyote wanayopenda kuipata hapa,”  amesema Rais Katalin

Sambamba na hayo Katarin ambaye ni Rais wa kwanza mwanamke nchini Hungary amesema Serikali yake imehakikisha wanafunzi wanaopata elimu nchini humo wanarejea nchini Tanzania ili kunuifaisha nchi kutokana na elimu wanayoipata.

Kwa upande wake Rais Samia amesema mwaka huu Tanzania itaanza kwa kusomesha wanafunzi watano kutoka Hungary, huku Hungary ikipanga kusomesha wanafunzi 30 kutoka nchini.

Itakumbukwa mwaka 2020 zaidi ya Watanzania 30 walifadhiliwa kwenda kusoma katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Hungary kwa muda wa miaka mitatu 2021/23.

Ziara hiyo ya Rais wa Hungary nchini inatarajiwa kumalizika Julai 20 mwaka huu ambapo leo atatembelea ubalozi wa heshima uliopo Kawe jijini Dar es salaam na kisha kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo jijini Arusha.

Hii ni ziara ya pili kubwa kufanywa na kiongozi mkuu wa nchi, ambapo imetanguliwa na ile iliyofanyika Machi 29 2023, ambayo Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alifanya ziara yake ya kwanza ambayo ilitamatika Machi 31, 2023.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV