Shilingi yaimarika dhidi ya Dola ya Marekani

November 19, 2024 10:47 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani imeongezeka kidogo ndani ya mwezi mmoja, jambo litakalowapatia ahueni wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kiwango cha kununua Dola moja ya Marekani kimeshuka kwa shilingi 67.37 hadi Sh2,658.44 Novemba 19 mwaka huu kutoka Sh2,725.81 kilichorekodiwa Oktoba 18.

Hata katika soko la rejareja katika benki za biashara, Shilingi imeendelea kuimarika dhidi ya Dola. Viwango cha kubadili fedha za Benki ya NMB PLC vinabainisha kuwa Dola moja inauzwa Sh2,730 leo kutoka Sh2,740 mwezi mmoja uliopita.

Kuimarika kwa Shilingi kutasaidia kupunguza maumivu kwa wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa na huduma kutoka nje ambao hutegemea zaidi Dola ya Marekani kufanya malipo yao kimataifa.

Tumia viwango hivi leo kufahamu taasisi inayotoa ofa nzuri ya fedha za kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks