Tanzania yazindua kiwanda cha kuunganisha malori, matipa

Kinaweza kuunganisha magari 45 kwa siku moja. Kutoa zaidi ya ajira 2,000.

Haitakuwa rahisi kufikia lengo la asilimia 80 nishati safi ya kupikia - Rais Samia

Amesema ili kupunguza matumizi ya nishati zisizo salama nchini juhudi za pamoja zinahitajika.

Wanafunzi 10,000 wa diploma Tanzania kupewa mikopo 2024-25

Idadi hiyo imeongezeka kutoka wanufaika 8,000 waliopangwa kupatiwa mikopo katika ngazi hiyo ya elimu katika mwaka wa fedha wa 2023/24.

Serikali ya Tanzania kutumia zaidi ya Sh1.9 trilioni wizara ya elimu

Zaidi ya nusu ya bajeti ya miradi ya maendeleo kutumika kugharamia mikopo ya elimu ya juu. Kamati ya Bunge yaonya juu ya Serikali kutotoa fedha zilizoidhinishwa. Yasema inaathiri utekelezaji wa baadhi ya shughuli za wizara.

Sh600 bilioni zaongezwa bajeti ya uchukuzi 2024-25, matumizi ya kawaida yakifekwa

Serikali yaliomba Bunge kuidhinisha Sh2.73 trilioni kwa mwaka wa fedha wa 2024-25 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31 kutoka kiwango cha mwaka jana.