Watahiniwa wa kidato cha sita, ualimu kuanza mitihani Mei 6

Mwandishi Wetu 0611Hrs   Mei 05, 2024 Habari
  • Idadi ya watahiniwa wa kidato cha sita, ualimu yaongezeka.
  • Watahiniwa waonywa kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu.


Dar es Salam.Watahiniwa 113,504 wa kidato cha sita wanatarajiwa kuanza Mtihani wa Kuhitimu  Elimu ya Sekondari (ACSEE) kesho, ikiwa ni daraja muhimu litakalowawezesha kuendelea na hatua nyingine za kitaaluma ikiwemo vyuo vya juu na vya kati.

Mitihani ya kidato cha sita ambayo hupima maarifa,stadi na umahiri wa wanafunzi katika maeneo waliyojifunza kwa kipindi cha miaka miwili itafanyika katika mkoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar na kumalizika Mei 24, mwaka huu. 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) Dk. Said Mohamed aliyekuwa akizungumza na wanahabari jiji Dar es Salaam leo Mei 5, 2024 amesema idadi ya watahiniwa waliosajiliwa mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 6.19.

“Mwaka 2023 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 106,883 hivyo kwa mwaka huu kuna ongezeko la watahiniwa 6,621 sawa na asilimia 6.19 ukilnganisha na mwaka jana,” amesema Dk. Mohamed.

Kati ya watahiniwa waliosajiliwa mwaka huu 104,449 ni wa shule na 9,055 ni wa kujitegemea, watahiniwa wa shule waliosajiliwa wavulana ni 57,378 sawa na asilimia 55, wasichana ni 47,071 sawa na asilimia 45,2.

Kwa upande wa wathiniwa wenye mahitaji maalum baraza hilo imesema 232 wamesajiliwa kati yao 201 wana uoni hafifu, 16 wasioona na wenye ulemavu wa viungo vya mwili ni 15.


Soma zaidi:Kimbunga Hidaya chawatesa wavuvi nane baharini Dar es Salaam


Watahiniwa wa ualimu kikaangoni 

Jumla ya watahiniwa 11, 552 wa ualimu nao wataingia kikaangoni kwa wiki mbili kuanzia kesho hadi Mei 20 mwaka huu ambapo mitihani hiyo itamalizika.

Kati yao 2,766 ni wa ngazi ya stashahada na 8,786  ni ngazi ya cheti, kwa ngazi ya stashahada wanaume ni 1,634 sawa na asimia 59 na wanawake ni 1,132 sawa na asilimia 41.

Mwaka 2023 waliosajiliwa walikuwa 8,479, idadi inayofanya ongezeko la wahitimu 3,073 sawa na asilimia 36.24 kwa mwaka huu kulinganisha na mwaka jana.


Epukeni udanganyifu wa mitihani 

Dk. Mohamed amewataka watahiniwa, wamiliki wa shule kujiepusha na vitendo vya udanganyifu huku akitoa rai kwa wananchi kuripoti viashiria vya udanganyifu pale vinapotaka kujitokeza na kwamba litawachukulia wale wote wataojihusisha na vitendo vya udanganyifu.

“Watahiniwa wote wanapaswa kutoa taarifa  kwa msimamizi mkuu mara wanapoabaini uwepo wa udanganyifu katika kituo cha mtihani…

...Baraza halisita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajirishisha kuwa kuna ukiukwaji wa taratibu za mithani ambazo zinahatarisha usalama wa mitihani yetu ya kitaifa,” amesema Dk. Mohamed.

Related Post