Spika Tulia ashinda urais Umoja wa Mabunge Duniani.

October 27, 2023 12:09 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Anakuwa rais wa 31 kuongoza umoja huo.
  • Ni mwanamke wa tatu akitanguliwa na Najma Heptulla wa India na Gabriela Cuevas wa Mexico.
  • Ameshinda kwa kura 172 kati ya 3000 za wajumbe waliopiga kura.

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson Mwansasu ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) baada ya kupata kura 172 kati ya 300 zilizopigwa.

Waliokuwa washindani wa Dk. Tulia ni pamoja na Adji Diarra Mergane Kanouté, kutoka Senegal ambaye amepata kura 59, Catherine Gotani Hara wa Malawi (kura 61) na Marwa Abdibashir Hagi wa Somalia aliyepata kura moja pekee.

Pamoja na kuwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura, Dk Tulia aliyekuwa akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo leo Oktoba 27, 2023 jijini Luanda nchini Angola, amewaambia washiriki kuwa amepokea nafasi hiyo akitambua majukumu yaliyopo mbele yake.


Soma zaidi : DP World kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 30



Soma zaidi : Zifahamu kozi sita zitazopewa kipaumbele mkopo wa HESLB ngazi ya Diploma 2023 – 24


Dk. Tulia anakuwa Spika wa 31 wa IPU akipikea kijiti cha Duarte Pacheco, Spika wa Bunge la Ureno, ambapo amekamilisha utawala wake katika mkutano wa 147 uliofanyika Angola.

Kwa mujibu wa IPU, Dk Tulia ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini anakuwa mwanamke wa tatu kuongoza umoja huo, akitanguliwa na Najma Heptulla wa India aliyeongoza kati ya 1999 na 2002 na Gabriela Cuevas wa Mexico aliyeongoza kuanzia 2017 hadi 2020.

Hata hivyo, Tulia anakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuwa rais wa IPU ambaye atashikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa muda wa miaka 25 iliyopita urais wa IPU, umekuwa ukizunguka katika nchi za Misri, Hispania, India, Chile, Italia, Namibia, Morocco, Bangladesh, Mexico na Ureno.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks