Soko la Masumbwe: Kivutio cha utalii kwa wafanyabiashara Kanda ya Ziwa

June 18, 2021 9:18 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Lilianzishwa mwaka 1952 na ni maarufu kwa minada ya bidhaa.
  • Ni kiungo cha biashara katika mikoa ya Geita, Tabora, Kagera, Mwanza na Shinyanga. 
  • Ni soko la asili lililopo kwenye uwanja wa wazi likiwa na vibanda vya nyasi. 

Geita. Kutembelea maeneo mbalimbali usiyoyajua ama kufika iwe ndani au nje ya nchi ni moja ya shughuli ya utalii ambayo itakufungua macho kufahamu usiyoyajua kuhusu eneo husika.

Hivi karibuni, baadhi ya waandishi wa habari wa Nukta Habari (www.nukta.co.tz) walitembelea Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kwa shughuli maalum.

Katika matembezi yao katika wilaya hiyo iliyofunikwa kwa milima na mabonde yenye misitu na hali ya ubaridi kiasi walifanikiwa kutembelea soko la Masumbe ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mifugo.

Bidhaa nyingine ambazo zinauzwa na wakazi na wageni katika soko hilo liko kwenye uwanja wa wazi ni mazao, bidhaa za nyumbani, mavazi na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika shughuli za uzalishaji. 

Soko hilo la asili ambalo vibanda vyake vimeezekwa kwa majani lilianzishwa mwaka 1952 limekuwa kiungo muhimu cha biashara katika mikoa ya Geita, Tabora, Kagera, Mwanza na Shinyanga. 

Wakulima na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Wilaya hiyo wamekuwa wakileta bidhaa katika soko hilo huku siku muhimu ikiwa ni siku ya Jumatano ambayo ni maalum kwa mnada.

Siku hiyo watu hufurika ili kujipatia mahitaji mbalimbali. Hizi ni baadhi ya picha ambazo zinaonyesha mandhari ya soko hilo ambalo linaweza kukuvutia kutembelea siku zijazo:

Wakati wa asubuhi wafanyabiashara wa soko hilo hujiweka tayari kwa kupanga bidhaa zao sokoni hapo. Picha| Gift Mijoe.

Kwa wapenzi wa kabichi basi hawatojutia kutembelea soko la Masumbwe. Picha| Gift Mijoe.

Mbogamboga na viungo vya kupikia navyo si haba sokoni hapo. Picha| Gift Mijoe.

Wakati huu ambao shule zimefunga, watoto nao huwasaidia wazazi kuuza matunda ili kujipatia kipato cha kuendesha familia. Picha| Gift Mijoe.

Kwa wapenzi wa miwa hawataondoka watupu katika soko la Masumbwe. Picha| Gift Mijoe. 

Wanamasumbwe hawajawasahau wapenzi wa mihogo. Picha| Gift Mijoe.

Kama shida bi vitunguu kukamilisha mapishi yako, basi sokoni Masumbwe ndiyo nyumbani. Picha| Gift Mijoe.

Wanamasumbwe katika pilikapilika kuhakikisha wateja wao hawazikosi huduma pindi wafikapo sokoni hapo. Picha| Gift Mijoe.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV