Serikali yaeleza gawio la Sh36.1 bilioni kutoka CRDB likavyotumika

June 30, 2022 6:54 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba (wa pili kulia), akipokea mfano wa hundi kifani yenye thamani ya Sh19.7 bilioni ikiwa ni sehemu ya gawio la Sh36.1 bilioni ambazo benki ya CRDB imetoa, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma Juni 30. Picha| Wizara ya Fedha na Mipango.


  • Imepata fedha hizo kwa sababu inamiliki hisa katika benki hiyo.
  • Imesema itatumia fedha hizo kutekeleza miradi ya maendeleo.
  • CRDB yasema gawio hilo limegawanywa katika taasisi mbalimbali za Serikali.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema gawio la Sh36.1 bilioni kutoka Benki ya CRDB litatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya na miundombinu.

Gawio hilo ambalo ni kwa mwaka 2021 limetokana na uwekezaji ambao Serikali imefanya ndani ya benki hiyo ya biashara kwa kushirikiana na mfuko wa uwekezaji wa pamoja na Serikali ya Denmark (DANIDA) pamoja na taasisi na mashirika mbalimbali ya umma.

Dk Nchemba aliyekuwa akizungumza Juni 29, 2022 jijini Dodoma amesema fedha hizo zimekuja kwa wakati mwafaka baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kwamba fedha hizo zitasaidia kutekeleza bajeti hiyo.

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha na kuweka mazingira rafiki na endelevu ya kufanya biashara katika sekta ya fedha ili kuiwezesha sekta hiyo kutoa mikopo kwa sekta za uzalishaji ili kutoa mikopo yenye riba nafuu itakayowezesha kuongeza uzalishaji na ajira kwa wananchi.  


Soma zaidi: 


Serikali ndiyo mwanahisa mkubwa ndani ya CRDB kwani ina hisa asilimia 21.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema gawio hilo la Sh36.1 bilioni kwa Serikali limegawanywa kwa taasisi zake ambapo Mfuko wa Ushirikiano wa Serikali na DANIDA umepata Sh19.7 bilioni, Mfuko wa Hifadhi kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) (Sh11.8 bilioni), Mfuko wa Hifadhi ya Taifa (NSSF) (Sh501.9 milioni na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) umepata Sh827.2 milioni.

Aidha, uwekezaji kupitia Serikali za Mitaa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo wa Lindi umepata Sh535.5 milioni, Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga (Sh5.8 milioni), Manispaa ya Shinyanga (Sh60.2 milioni) na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imepata Sh3.2 milioni.

Halmashauri zingine zilizopata mgao ni pamoja na Wilaya ya Chunya na Rungwe pia Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Umoja Fund Unit Trust Scheme na Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi.

Benki ya CRDB imeendelea kuimarika na kuongeza faida kila mwaka na kusababisha kuongezeka kwa gawio la wanahisa kutoka Sh22 kwa hisa moja kwa mwaka 2020 hadi Sh36 kwa mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 64.

Juni 3, Serikali Serikali ilivuna gawio la Sh4.5 bilioni kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kutokana na faida iliyopata benki hiyo mwaka 2020/21 ambapo inamiliki asilimia 30 ya hisa za benki hiyo. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV