Serikali yaahidi mazingira rafiki kuongeza idadi ya redio Tanzania

February 13, 2020 10:59 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Dk Mwakyembe amesema Serikali itaendelea kuenzi mchango na kazi nzuri inayofanywa na vituo vya redio nchini

Dar es Salaam. Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uanzishaji wa redio nyingi zaidi nchini ili kuenzi mchango wa redio hapa Tanzania. 

Dk Mwakyembe ameeleza leo (Februari 13, 2020) katika taarifa iliyotolewa na wizara yake kuwa redio zimekuwa zikifanya kazi nzuri zenye mchango mkubwa kwa Taifa. 

“Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi mchango na kazi nzuri inayofanywa na redio hapa nchini ikiwemo kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uanzishaji wa redio nyingi zaidi,” amesema Dk Mwakyembe katika ujumbe wake wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani. 

Siku ya redio ulimwenguni huadhimishwa kila mwaka baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kuitangaza rasmi Februari 13, 1946ili kuelimisha na kuhamasisha umuhimu wa redio.  Siku hiyo ndiyo redio ya umoja wa mataifa ilianzishwa. 


Zinazohusiana:


Hadi kufikia Februari 12, 2020, waziri huyo amesema Tanzania ilikuwa na  vituo vya redio 204 vilivyosajiliwa hapa nchini vikiwemo 21 vya masafa ya mtandaoni (online radio) hali inayowafanya Watanzania kupata haki yao ya msingi ya kikatiba. 

Wadau mbalimbali wa redio nchini nao wameeleza namna redio zilivyosaidia kubadilisha maisha yao ikiwemo kuwapa ajira.

“Redio imebadilisha maisha yangu. Redio imenisaidia kutafuta wito wangu. Ntazidi kuipenda redio,” amesema Michael Baruti, mwanahabari wa Shirika la habari la Uingereza (BBC) kupitia ukurasa wa Twitter.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV