Mikopo halmashauri kuanza kutolewa tena Novemba 2024, bilioni 79 zikiwa hazijarudishwa

October 30, 2024 1:04 pm ยท Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yatenga Sh227 bilioni kwa ajili a mikopo hiyo.ย 
  • Bunge la Tanzania limeazimia Sh79 bilioni zirejeshwe kablaย  ya Juni 30, 2026.

Arusha. Wakati Serikali ya Tanzania ikitarajia kuanza kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuanzia Novemba 30, 2024 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imebaini Sh 79.7 ya mikopo hiyo haijarejeshwa.

Mwaka 2018 Serikali ilipitisha sheria iliyozielekeza Serikali za Mitaa nchini kutenga asilimia10 zaย  mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake kwa asilimia 4, vijana asilimia 4 na walemavu asilimia 2.

Fedha hizo zilitazamiwa kuwezesha vikundi hivyo kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo itakayowainua kiuchumi.

Hata hivyo, Aprili 13, 2023 Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alitangaza kusitishwa kwa mikopo hiyo ili kupisha utaratibu mwingine wa utoaji wa mikopo hiyo baada ya ule wa awali kukumbwa na changamoto lukuki ikiwemo wakopaji kutokufanya marejesho.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Festo Dugange aliyekuwa akizungumza wakati wa maswali na majibu bungeni jijini Dodoma jana Oktoba 29, 2024 alisema uchambuzi wa awali umeshaanza kufanyika na mikopo hiyo itaanza kutolewa Novemba mwaka huu.

โ€œMafunzo yanaendelea kutolewa kwa kamati za usimamizi wa huduma ya mikopo ngazi ya kata, halmashauri, wilaya pamoja na vikundi. Kufuatia matunzo yaliyotolewa uchambuzi wa awali mikopo umeshaanza katika ngazi ya Serikali za Mitaa na mikopo hiyo inatarajiwa kutolewa kabla au ifikapo Novemba 30, 2024,โ€amesema Dugange.ย 

Ahadi hiyo ni tofuati na ile aliyoitoa Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Tamisemi Aprili 16, 2024 aliyetangaza kurejeshwa kwa mikopo hiyo Julai mwaka huu alipokuwa akisoma bajeti yake kwa mwaka 2024/25.

Waziri huyo alisema Serikali imetenga Sh227.9 bilioni wa ajili ya mikopo hiyo huku Sh63.67 bilioni kati ya fedha hiyo ikiwa ni fedha za marejesho ya mikopo ya awali.

Mikopo hiyo itaanza kutolewa mwezi ujao huku kukiwa na deni la Sh79.7 bilioni ambalo wakopaji wa mikopo hiyo katika awamu zilizopita hawakurejesha.

Halima Mdee Mwenyekiti wa LAC aliyekuwa akizungumza wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka 2023 amesema fedha hizo ni zile ambazo muda wake wa marejesho umeisha.

โ€œHii 79 (bilioni) tunayaoizungumza ni ile mikopo chechefu ambayo muda wake wa kimkataba umeisha haijakusanywa na hakuna mkakati madhubuti wa kukusanya,โ€ amesema Mdee,

Amezitaja halmashauri zilizoshindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati kuwa ni pamoja na Kinondoni Sh6.1 bilioni Temeke Sh5.3 bilioni na Ubungo Sh4.8 bilioni.

Kufuatia ripoti ya kamati hiyo, Bunge la Tanzania limeazimia kurejeshwa kwa mikopo hiyo iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kablaย  ya Juni 30, 2026.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW