Serikali imesema imeajiri walimu zaidi ya 14,000 ndani ya miaka miwili
- Mbunge wa jimbo la Madaba, Joseph Mhagama amehoji kwanini Serikali isiwe inasomesha walimu kulingana na mahitaji ya soko.
- Serikali imesema imeajiri walimu 14,422 ndani ya miaka miwili ya hivi karibuni.
Dar es salaam. Serikali imesema imeajiri walimu 14,422 ndani ya miaka miwili ya hivi karibuni huku ikieleza kuwa haitasita kusomesha wanafunzi wanaosomea taaluma ya ualimu licha ya kuwa wengi ili kuwapatia wigo mpana wa fursa za ajira na kujiajiri.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais- Tamisemi Mwita Waitara ameeleza leo bungeni kuwa kati ya walimu hao waliojiriwa kati ya mwaka 2017/18 na 2018/19, takriban robo tatu au walimu 10,695 waliajiriwa shule za msingi na 3,727 waliosalia wanafundisha shule za sekondari.
Waitara alikuwa akijibu swali ya mbunge wa Mbinga, Martin Msuha aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali kupeleka walimu wa masomo hayo wilayani Mbinga baada ya kuwepo uhaba wa walimu wa hisabati na sayansi uliyoathiri zaidi zaidi matokeo ya masomo hayo.
Akijibu swali hilo, Waitara amesema zipo sababu nyingi zilizosababisha kushuka ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba wilaya ya Mbinga ikiwemo upungfu wa walimu, utoro na ushiriki hafifu wa wazazi katika kufutilia masomo ya elimu ya watoto wao.
Zinazohusiana:
Shule zinavyochuana kubaki katika 10 bora kidato cha sita
“Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepatiwa walimu 143 ambapo walimu 112 ni wa shule msingi na walimu 31 wa shule za sekondari,’’ amesema Waitara wakati akielezea mgawanyo wa walimu waliopelekwa Mbinga katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni.
Hata hivyo, katika swali la nyongeza Mbunge wa jimbo la Madaba, Joseph Mhagama amehoji kwanini Serikali isiwe inasomesha walimu kulingana na mahitaji ya soko badala ya inavyofanya sasa ambapo vijana wengi waliosomea ualimu wapo mtaani.
“Tunaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanafunzi hao badala ya kutegemea kuajiriwa tu na Serikali bali kuona watakavyoaanzisha kufanya kazi hata kwa shughuli binafsi,” amesema Waitara.
aitara amesema ni kweli kuna walimu wengi mtaani lakini ni kweli tunahitaji walimu katikshule zote za msingi na sekondari
Latest