Sehemu ya pili filamu ya “The Royal Tour” kuzinduliwa hivi karibuni

August 10, 2022 1:33 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Imepewa jina la “The Hiddden Tanzania.
  • Vivutio vya mikoa ya nyanda za juu kusini kupewa kipaumbele.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Suluhu amesema sehemu ya pili ya filamu ya “The Royal Tour” inatarajiwa kutoka hivi karibuni lakini itakuja kivingine ikilenga kuonyesha maeneo ya utalii yaliyojificha yaliyopo Tanzania.

Filamu hiyo ambayo ni mwendelezo ya kwanza itapewa jina la “The Hidden Tanzania”.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba mkoani  Njombe, leo Agosti 10, 2022 amesema awamu ya pili ya filamu hiyo itaonyesha vivutio ambavyo havikuonyeshwa kwenye awamu ya kwanza.

“Waandaaji wameipa jina la “The Hidden Tanzania” yaani maeneo mengine ya Tanzania yaliyojificha, ni kwenda kuyachukua na kuyaonyesha kwamba Tanzania mbali ya tuliyowaonyesha bado kuna mambo haya,” amesema Rais Samia.


Zinazohusiana:


Kumekuwa na malamiko kwamba filamu ya “The Royal Tour” imesahau vivutio vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini, ikiwemo mikoa ya Njombe, Mbeya, Songwe, Iringa na Songea.

Wakazi wa Njombe wamemuomba Rais Samia  Hifadhi ya Taifa ya Kitulo kuiingizwa kwenye mradi wa kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).

Akjibu hoja hiyo, Rais Samia amesema awamu ya pili ya filamu ya “The Royal Tour” itahusisha hifadhi hiyo kwa hiyo wasiwe na wasiwasi.

“Mikoa hii ya nyanda za juu kusini itaingia kwenye awamu ya pili ya  “The Hidden Tanzania” tuonyeshe vivutio vyetu na watalii waje wengi zaidi,” amesema Rais Samia.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
21 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV