Samsung inavyojiimarisha kibiashara Tanzania

March 17, 2022 8:00 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Afisa Mkuu wa Ubunifu na Mikakati wa Tigo, David Umoh akijifunza kuhusu vipengele vya simu ya mkononi ya Galaxy S22 kutoka kwa mwakilishi wa Samsung, Betty Shayo. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu mpya wa kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Tae Sun Lee na kushoto kwake ni Samuel Odhiambo: Mkuu wa Kitengo cha Watumiaji wa Samsung Afrika Mashariki na Charles Kimari ambaye ni Mkuu wa Uzoefu wa Simu wa Samsung Afrika Mashariki walishiriki mkutano wa Samsung uliofanyika Machi 16, 2022 jijini Dar es Salaam. 


  • Yawakutanisha wadau wakiwemo wafanyabiashara zaidi 100 jijini Dar es Salaam.
  • Wajadili namna ya kukuza uhusiano wa kibiashara na utoaji bidhaa bora.
  • Waingia makubaliano na Tigo kuwapatia wateja wake intaneti.

Dar-es-Salaam. Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki imekutana na kuzungumza na wadau wake wa kibiashara ili kuimarisha uhusiano na kujadili matumizi bora ya bidhaa zake kwa wananchi wa Tanzania. 

Kampuni ya Samsung inaamini kuwa maendeleo ya kiteknolojia ndiyo kichocheo kikuu cha biashara ya bidhaa zake ulimwenguni.

Mazungumzo hayo ambayo ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na wateja wake, yamefanyika Machi 16, 2022 katika hoteli ya Hayatt Jijini Dar es Salaam yakiwakutanisha wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa zake kutoka pande zote Tanzania.

Mkutano huo umeandaliwa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Tae Sun Lee na kuwaleta pamoja wadau wakuu wa bidhaa za Samsung wakiwemo wasambazaji na wafanyabishara ili kuhakikisha matumizi bora yanatolewa kwa watumiaji wa bidhaa za Samsung.

Mkurugenzi Mkuu wa Samsung, Lee amesema kuwa kampuni ya Samsung itaendelea kuimarisha uhusiano na washirika wake wakiwemo wasambazaji wote wa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki.

Lee amesema kuwa Samsung itahakikisha bidhaa zote zinazotengenezwa na kampuni hiyo zinaendelea kuwa zenye ubora wa hali ya juu ili kumpa furaha na faraja mtumiaji wake.

“Kama Samsung tunasisitiza kuwa tutaendelea kuwa na sauti moja pale tunapoweka mikakati yetu ili tuweze kwenda mbele. Mienendo yetu ya soko inaendelea kubadilika na pia tunaona haja ya kurekebisha katika maeneo mbali mbali ili kukidhi mahitaji ya wadau,” amesema Lee.

Aidha, amesema mkakati wa kampuni hiyo ni kuona bidhaa zake za kielektroniki zinaendelea kukubalika katika soko la Afrika.

Katika mkutano huo, bidhaa mbalimbali za kampuni ya Samsung za mwaka 2022 zimeonyeshwa zikiwemo simu.


Soma zaidi:


Fursa zaidi 

Katika mkutano huo, kampuni ya mawasiliano ya Tigo, wameanzisha ushirikiano na Samsung ikiwa ni mpango kabambe wa kumuwezesha mteja anayetumia runinga ya Samsung (Smart TV) kupata kifaa cha intaneti (Mi-Fi) kutoka Tigo.

Mteja atakayenunua runinga ya Samsung katika kipindi cha ofa ataweza kupata kifaa hicho cha MiFi kikiwa na kifurushi cha kuanzia ili kumuwezesha kujiunga na mtandao wa intaneti katika runinga yake.

“Kama Tigo, kupitia teknolojia tunalenga kufanya maisha ya Mtanzania kuwa bora zaidi, ndiyo maana tumeamua kushirikiana na kampuni ya Samsung katika kuhakikisha kila mteja atakayenunua Smart TV ya Samsung anapata kifaa cha intaneti cha MiFi kutoka Tigo,” amesema Afisa Mkuu wa Mikakati na Ubunifu wa Tigo, David Umoh. 

Umoh amesema Samsung imekuwa mmoja wa washirika wao wakuu nchini Tanzania na amesisitiza kuwa wataendelea  kufanya kazi pamoja ikiwa ni katika mipango chanya ya kuhakikisha maisha ya Mtanzania yanakuwa bora zaidi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo wakiwemo wafanyabiashara zaidi ya 100 waliokutana na kujadili mahitaji ya soko na jinsi gani kwa pamoja wanaweza kukuza soko la Samsung nchini Tanzania.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...