Kunani uzinduzi wa Samsung mwaka 2022?

February 9, 2022 1:37 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inatarajia kufanya uzinduzi wa bidhaa mpya leo.
  • Bidhaa hizo ni pamoja na simu mpya za Samsung Galaxy 22, tableti na vifaa vya kusikilizia muziki.
  • Hafla hiyo itaonyeshwa mtandaoni mubashara.

Dar es Salaam. Baada ya simu zingine kuingia sokoni, namaanisha OnePlus toleo la 10 na zinginezo, sasa ni zamu ya Samsung kugonga hodi sokoni.

Kampuni hiyo ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki Zikiwemo simu na bidhaa za jikoni inatarajia kuzindua bidhaa zake mpya za mwaka 2022 katika hafla ya mtandaoni ya Samsung Unpacked 2022.

Licha ya kuwa zimebaki saa chache kuelekea katika shughuli hiyo inayofanyika leo Februari 9, 2022, haya ndiyo tunayoyatarajia kutoka kwa Samsung.

Uzinduzi wa Samsung Galaxy S22 na Galaxy S22 Ultra

Katika kila hafla ya uzinduzi inayoandaliwa na Samsung, matoleo mapya ya simu hutangazwa. Kwa mwaka 2022, tunatarajia Glaxy22 na 22 Ultra.

Za chini ya kapeti kutoka kwa wadau wa teknolojia wakiwemo Toms guide ni kuwa, simu hizo zitaanza kuwekewa oda (pre order) mara tu baada ya hafla kuisha huku tarehe inayotarajiwa simu kuwa sokoni ikitajwa na mdau wa teknolojia, Ishan Agarwal kuwa ni Februari 25 mwaka. 

Mbali na simu hizo mbili, tunatarajia kuja kwa tableti ya Galaxy Tab S8 na huenda tukapata miundo mingi katika mpambano wa Samsung na iPad Pro

Zinazovuma ni kuwa, S22 inasadikika kuwa simu ambayo kioo chake (display) kina mwanga zaidi katika historia ya simu na kuiacha iPhone13 nyuma. Kamera ya S22 inayoanzia MegaPixel (MP) 108 ni kamera inayotajwa kunasa picha zenye muonekano mzuri zaidi.


Soma zaidi


Teknolojia mpya ikiwemo aina mpya za lensi (super clear lens) inayopunguza mwanga unaoaksiwa itasaidia kuboresha picha zinazotokana na simu hizo.

Kwa upande wa gharama, simu hizi zi zinatarajiwa kuongeza gharama ikilinganishwa na S21 ya mwaka jana. Tomsguide inaainisha kuwa, ongezeko la gharama linatarajiwa kuwa kati ya Sh132,177 hadi Sh231,150.

Kwa upande wa Galaxy Tab S8 Ultra, wadau wanasema mtumiaji ambaye ni mchoraji ataweza kutumia  simu ya Galaxy S22 Ultra kama kibao cha rangi yaani “color palette” wakati wa kuchora. Kitu ambacho ikilinganishwa na iPad Pro, Tab S8 inakuwa imetusua anga.

Vifaa vingine vya kielektroniki tutakavyoviona ni pamoja na “wireless earbuds”.

Hafla ya uzinduzi itaonyeshwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Samsung, YouTube na kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, TikTok na  Twitter.

Nini kitajiri? Tutakuja hapa hapa kukujuza.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...