Safari ya mwisho ya Mengi kuhitimishwa Mei 9

May 3, 2019 12:09 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwili wa marehemu Renald Mengi utawasili jumatatu ya Mei 6 jijini Dar es Salaam na Mei 9 atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Machame mkoani Kilimanjaro. 
  • Ataagwa Mei 7 katika ukumbi wa Karimjee.

Dar es Salaam. Safari ya mwisho ya kumpumzisha katika nyumba yake ya milele marehemu Reginald Mengi itahitimishwa siku ya Alhamis ya Mei 9 mwaka huu machame mkoani Kilimanjaro. 

Mengi aliyekuwa mfanyabiashara na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP,  alifariki dunia akiwa mjini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Aprili 3, 2019) na Mwanasheria wa familia ya Mengi,  Michael Ngalo mwili wa marehemu utawasili Jijini Dar es Salaam jumatatu ijayo (Aprili 6, 2019) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na baadaye utapelekwa katika hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa. 

Ngalo amesema siku inayofuata ya Mei 7, mwili wa marehemu utatolewa Lugalo na kupelekwa katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kuagwa na jioni mwili utalala nyumbani kwake Kinoindoni. 


Soma zaidi:


Mei 8 ambayo itakuwa siku ya jumatano mwili utasafirishwa kwa ndege hadi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na moja kwa moja utapelekwa nyumbani kwake Machame kwa ajili ya taratibu nyingine za maziko. 

Hatimaye safari yake ya mwisho ya kumpumzisha marehemu katika nyumba yake ya milele itahitimishwa Machame Mei 9 baada ya misa katika kanisa la KKKT, Kisereni.   

Mengi atakumbukwa kwa mengi hasa mchango wake katika kuimarisha na kuendeleza tasnia ya vyombo vya habari nchini.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW