Sababu za ndege ya Air Tanzania kuachiwa Afrika Kusini

September 4, 2019 10:56 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema mahakama ya Gauteng ya nchini Afrika Kusini leo Septemba 4, 2019 imeamuru ndege ya Air Tanzania (ATCL) Airbus A220-300 iliyokuwa inashikiliwa nchini humo kuachiwa. 

Mahakama hiyo imeamtaka raia wa Afrika Kusini, Hermanus Steyn aliyefungua kesi akitaka kulipwa Dola za Marekani milioni 33 kulipa gharama za kesi hiyo baada ya kushindwa. 

“…Hoja zote zilizotolewa na mawakili wetu zimeshinda, na tumeshinda kesi hiyo, na imeamriwa ndege hiyo #AirTanzania iweze kuondoka,”  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Dk Damas Ndumbaro. 

Ndege hiyo ilizuiliwa  tangu Agosti 23, 2019 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wa Johannesburg  imezuiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg, jambo lililoibua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii.

Akitoa taarifa rasmi ya Serikali, leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ni kweli ndege hiyo imeachia rasmi na itaendelea na shughuli zake za kawaida. 

“Ndege yetu Airbus ya ATCL ambayo ilikuwa imeizuiliwa Afrika Kusini ikiwa katika shughuli zake leo imeachiwa rasmi. Inarudi katika aratiba zake za kawaida,” amesema Waziri huyo. 

Amebainisha kuwa Watanzania wanaipenda ndege yao na sasa itarudi huku akiweka wazi kuwa Serikali iko mbioni kununua ndege nyingine. 

“Nashukuru nilikuwa na tenson kubwa, Watanzania wanapenda kupanda ndege ya kwao ya ATCL. Kwa hiyo ratiba ile iliyokuwa inayumba yumba ndugu zangu Watanzania sasa inarudi. Tunaendelea na ununuzi wa ndege nyingine mbili. Tupo vizuri,” amesema.

Enable Notifications OK No thanks