Zingatia haya wakati wakupanga sherehe yako
- Hakikisha unafurahia sherehe yako
- Epuka mikopo isiyo ya lazima
- Kuwa mbunifu
Dar es Salaam. Unatarajia kuwa na sherehe hivi karibuni? “Baby shower” Arobaini ya mtoto, Sherehe ya kuaga ukapela, ”Kitchen party” “Send off” ama Harusi? Basi huenda kichwani umejaa mawazo ambayo mara kadhaa yanakukosesha hata usingizi.
Maswali ya “pesa nitatoa wapi”, “je nitafanikiwa”, “vipi ikinyesha mvua” yanaweza kuwa ni kati ya maswali machache yanayo zunguka akilini mwako.
Zingatia dondoo hizi kwaajili ya kufanya shughuli yako kuwa yenye kumbukumbu nzuri na zaidi, kuwa shughuli uliyoifurahia.
- Kabidhi shughuli yako kwa mtaalamu
Mara nyingi unashindwa kufurahia sherehe yako kwasababu umeshikilia kila kitu. Baadhi ya watu huingilia kamati na kutaka kujua kila lililo nyuma ya pazia lakini, hata kamati kwa sasa inakuwa ni masuala yanayopitwa na wakati kwani wapo wataalamu wa sherehe ambao wanaweza kukusaidia kufanya sherehe ambayo ipo kwenye bajeti yako.
“Event planners” ni watu wa kuangazia kipindi cha sheehe yako na kama unaona ni shida kuwapata, unaweza ukachagua hata afikia au mtu unaye mwamini aweze kusimamia kila kitu badala yako kwa kuwa unahitaji kuifurahia siku yako.Maswali ya “pesa nitatoa wapi”, “je nitafanikiwa”, “vipi ikinyesha mvua” yanaweza kuwa ni kati ya maswali machache yanayo zunguka akilini mwako. Picha| Entrepreneur.com
- Weka fedha kwa ajili ya dharura
Kama shughuli yako ina bajeti ya Sh10 milioni, unaweza kuweka hata Sh2 milioni au zaidi kwaajili ya dharula.
Mara nyingine dharura zinaweza kutokea na hivyo kuhitaji kufanya maamuzi magumu na ya haraka.Mfano, sherehe yako inafanyika kwenye bustani na ghafla mvua ikanyesha. Kwa kutumia fedha ya akiba, unaweza kukodi mahema au hata kulipia sehemu kwaajili ya kukamilisha sherehe yako.
- Fungamana na bajeti yako
Hakuna haja ya kuingia kwenye mikopo kwaajili ya kuridhisha wageni waalikwa. Mtu anayestahili kuridhika ni wewe. Hivyo, ni vizuri ukafungamana na kiasi cha fedha ulichonacho kwaajili ya kufanya sherehe yako ilihari vitu vya muhimu kama vinywaji, chakula na menginyo yamefikiwa.
Kukopa kwaajili ya sherehe ya masaa machache inaweza kukuumiza kichwa baadaye na hata ulio wafurahisha wasiweze kukusaidia kulipa madeni uliyonayo.
Zinazohusiana
- Bajeti inavyookoa matumizi mabaya ya fedha ngazi ya familia
- Mambo ya kufanya wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka
- Kuwa mbunifu
Kutokanana sherehe kuwa nyingi, ratiba za sherehe zimekuwa zikifanana. Mathalani kwa harusi, imezoeleka ni kuingia wageni waalikwa, kuingia maharusi, utambulisho, keki na champain chakula, mawaidha kutoka kwa wazazi na kisha mwisho wa sherehe.
Una nafasi ya kuweka sukari kidogo kwenye sherehe yako ili iwe ya tofauti na uifurahie zaidi. Umewahi kuwaza kuwa unaweza kuingia ukumbini kwa namna tofauti? Au kama unaweza kuonda mawaidha na risala na kuweka burudani ili watu washereheke zaidi kwani wageni waalikwa huenda hata hawasikilizi.
- Furahia siku yako
Hauna haja ya kuwa na mawazo kiasi cha kusema “bora imeisha” pale sherehe yako ikishapita. Weka kila namna ya kufurahia sherehe yako kwani haitajirudia mara mbili au zaidi.
Unaweza kufikia hatua hii kwa kuzingatia hatua zilizoainishwa hapo juu.
Ni muhimu kufurahia nyakati hizo na uwapendao. Picha| Mtandao
Sherehe ni kitu muhimu kwa mwanadamu. Una kila sababu ya kufurahia mafanikio yako kwani umepitia mengi kuyafanikisha.
Ni muhimu kufurahia nyakati hizo na uwapendao na zaidi kuhakikisha unaifurahia haswa kwani, itakupa ari ya kufanya mambo mengine kwa uweledi ili ushreheke hapo yatakapo fanikiwa.
Nukta Habari (www.nukta.co.tz) inakutakia kila la kheri kwenye sherehe yako.