Walimu wageuka mateka katika nchi yao

January 28, 2022 6:34 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni walimu wa nchini Honduras wanaolengwa na makundi ya uhalifu.
  • Wengine wafanyiwa vitendo vya unyanyasaji kijinsia.

Dar es Salaam. Mwanzoni mwa kila mwaka mpya wa shule, wakati maeneo mengine duniani walimu na wanafunzi hufurahia shule funguliwa, walimu wa nchini Honduras hali huwa ni tofauti.

Hupatwa na hofu wakikaa kusubiri maagizo sio kutoka serikalini bali katika magenge ya wahalifu ya namna ya kuendesha shughuli zao shuleni.

“Wavulana huja kila tunapoanza mwaka wa shule, na wanawasiliana nami ili kunijulisha miongozo ambayo watatupa kuhusu uendeshaji wa shule katika mwaka,” mmoja wa walimu nchini humo, Horacio Montes kuhusu magenge ya uhalifu yalivyofanikiwa kuingilia elimu katika hiyo ndogo iliyopo Amerika ya Kati,

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limesema walimu nchini Honduras wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na ghasia za magenge ya wahalifu na sasa walimu wanatambuliwa kuwa moja ya makundi yenye uwezekano mkubwa wa kulazimika kuyakimbia makazi yao.

Maisha ya walimu hao yamekuwa magumu kwani wengine hulazimika kutoa hongo ili waende kazini, huku wakitafuta pesa kila mara wanapovuka mipaka isiyoonekana inayotenganisha maeneo ya magenge.

 “Kuna wakati tunaweka maisha yetu rehani, na miili yetu katika hatari ili kuwalinda wavulana na mabinti zetu. Tunaweza kusema kwamba ‘tunabeba mzigo’, lakini hatuna ulinzi sisi wenyewe,” Mwalimu Mkuu, Miguel Lopez wa shule moja huko Honduras.

Aidha, walimu wa kike wako katika hatari zaidi, kwani wanaweza kulengwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na kushambuliwa na vijana wa magenge ya uhalifu.


Soma zaidi:


Mwalimu Mkuu msaidia katika shule moja ya awali,  Alba Flores amesema “tunatafuta njia za ulinzi sisi wenyewe, kwa ajili ya wenzetu, wanafunzi na wakati mwingine, kwa wazazi. Daima tutakuwa marafiki zao watoto, tunawapenda, na tunafanya kazi kwa ajili yao.”

Uchunguzi wa UNHCR na shirika linalowakilisha walimu wa shule wa Honduras Comité Docent pamoja na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children, uliofanyika mwaka 2016,  ulibainisha walimu kuwa miongoni mwa makundi nchini Honduras ambayo huathirika zaidi na kulazimishwa kuyakimbia makazi yao.

Walimu wa Honduras wanajikuta kwenye mstari wa mbele wa wakimbizi wa ndani ambapo zaidi ya watu 247,000 wameyakimbia makazi yao.

Wadau wa elimu wamekuwa yakifanya kazi pamoja tangu mwaka 2016 kutafuta suluhu za matatizo yaliyokita mizizi ya walimu ili kuwaweka katika kazi zao na jamii zao nyumbani, lakini pale baadhi ya walimu wanapokuwa katika hatari zaidi hupelekwa UNHCR, ambayo inafanya kazi ya kuwahamishia kwenye usalama zaidi ikiwa ni ndani au nje ya Honduras.

Enable Notifications OK No thanks