Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kufikia Sh81.86 bilioni mwaka 2025/2026

April 25, 2025 4:05 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Bajeti hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuendeleza miradi ya uchumi wa buluu nchini.
  • Fedha hizo zitaelekezwa katika mishahara, matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi muhimu ya mazingira.

Dar es Salaam. Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) imeomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh81.86 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni aliyekuwa akisoma hotuba ya bajeti leo Aprili 25,2025 ameeleza kuwa kati ya kiasi hicho Sh61.91 bilioni zimetengwa kwa ajili ya fungu 31 ambapo Sh19.9 bilioni ni kwa matumizi ya ofisi binafsi ya Makamu wa Rais.

Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) imeomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh61.91 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo.

Mwenyekiti wa Bunge, Deodatus Mwanyika akiongoza kikao cha kumi na mbili cha mkutano wa kumi tisa wa Bunge. Picha/ Bunge la Tanzania/ x.

“Kati ya kiasi kinachoombwa kwa Fungu 26, Sh10.6 bilioni ni kwa ajili ya mishahara na Shi18.8 bilioni ni matumizi mengineyo,” amesema Waziri Masauni.

Akifafanua zaidi, Waziri Masauni amebainisha kuwa fungu 31 linahusisha matumizi ya kawaida ya Sh28.8 bilioni. 

Kati ya fedha hizo, Sh10.90 bilioni ni mishahara ya wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), huku Sh17.9 bilioni zikielekezwa katika matumizi mengineyo.

“Aidha, fedha za miradi ya maendeleo zinajumuisha Sh46.02 bilioni fedha za ndani na Sh28.45 bilioni ikiwa ni fedha za nje,”amefafanua Waziri Masauni.

Bajeti hiyo ya mwaka 2025/26 inaonyesha ongezeko la asilimia 18.36 kwa matumizi ya kawaida na asilimia 41 kwa miradi ya maendeleo ikilinganishwa na Sh45.7 bilioni zilizoombwa na wizara hiyo mwaka wa fedha 2023/24.

Kwa upande wa miradi ya maendeleo imeongezeka kwa asilimia 18.36 wakati kwa upande wa wa miradi ya maendeleo ikiongezeka kwa asilimia 41 ukilinganisha na mwaka wa fedha 2024/2025.

Kwa mujibu wa Dk Oscar Ishengoma Kikoyo aliyekuwa akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria amebainisha kuwa ongezeko hilo limechangiwa na upandaji wa bei za bidhaa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2025/26. Picha/ Bunge la Tanzania/x.

Hata hivyo, kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Ofisi ya Makamu wa Rais imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo: kusimamia utawala na menejimenti ya rasilimali watu, kuratibu uandaaji wa maandiko na nyaraka rasmi za ofisi na kuandaa mipango na bajeti pamoja na taarifa za utekelezaji wa mipango. 

Pia, shughuli nyingine ni kutoa elimu kwa umma kuhusu sera, mikakati na majukumu ya ofisi pamoja na kuendeleza uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira na kuratibu shughuli za uchumi wa buluu.

Vipaumbele 

Waziri Masauni amebainisha kuwa sehemu kubwa ya bajeti itaenda kwa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi wa mazingira huku miongoni mwa miradi hiyo ikiwa ni mradi wa urejeshaji wa mazingira bonde la Rukwa na Ruaha ambapo utagharimu Sh7.1 kwa ujenzi wa malambo na urejeshaji wa ardhi.

Miradi mingine ni  Mradi wa uhimilivu wa tabianchi Kigoma utakaogharimu Sh17.0 bilioni kwa ukarabati wa mifereji na upandaji wa miti hekari 12,000.

Vilevile, mradi wa kuzuia uharibifu wa tabaka la ozoni utakaogharimu kiasi cha Sh433 milioni 433 pamoja na mradi wa uhifadhi wa ziwa Babati, Chala na Jipe utakaogharimu kiasi cha Sh200 milioni kwa kila ziwa kwa kupanda miti na kuelimisha jamii.

Endapo bajeti hiyo itaidhinishwa na Bunge, Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa katika kulinda rasilimali zake za asili, kuimarisha mshikamano wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks