Vitu vya kuepuka unapokua na huzuni

September 23, 2020 6:20 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanadamu wote wameumbiwa kupita katika vipindi vya huzuni na furaha.
  • Unapokuwa katika huzuni, changamana na watu na sikiliza nyimbo za hamasa.
  • Kumbuka majonzi na huzuni vinasaidia kujenga ukomavu wa kifikra.

Dar es Salaam.  Siku chache zilizopita nilikuwa furaha yangu ilizimika kama mshumaa uliotelekezwa nje kwenye upepo. Nilihisi dunia yote imenigeuka, hivyo sikua na sababu ya kutabasamu wala kuigiza furaha.

Nilimpoteza mtu muhimu katika maisha yangu. Hali hiyo ilinipelekea kujihisi mnyonge na mwenye huzuni na katika kipindi chote hicho.

Nilifanya mambo ambayo yaliyozidisha huzuni yangu. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanapitia kipindi kama changu, nakushauri usifanye mambo haya ili ufanikiwe kuirejesha furaha yako kwa haraka:

Usipendelee kukaa peke yako

Katika kipindi hiki, nilipendelea kuwa peke yangu na kujifungia ndani ili nisisikie salamu za pole kwani zilinikumbusha juu ya mpendwa wangu na hivyo kuibua hisia za huzuni. 

Nilijikuta nikitumia muda mwingi kulalamika kwanini Mungu amemchukua mapema kuliko kupanga mipango ya nini nifanye baada ya kuondoka kwake.

unapokaa peke yako unachochea msongo wa mawazo. Picha| Freepik.

Sikiliza maudhui yanayokutia moyo

Baadhi ya watu wanapokuwa wametendwa na wapenzi wao, husikiliza nyimbo za kuvunjika moyo zinazoendana na hali yao. 

Kwa upande wangu, wimbo wa “Baadaye” wa Amos na Josh ulinisaidia kurejesha furaha yangu iliyopotea kwa muda. Nilichokuwa sifahamu ni kuwa nilikuwa nikichochea simanzi zaidi kuliko kutafuta amani ya moyo.

Kwa waliopo kwenye mahusiano, pale unapoumizwa, epuka kusikiliza nyimbo za kuumiza na badala yake, sikiliza nyimbo za matumaini. 

Usione kuwa tatizo lako ni kubwa kuliko mengine

Baadhi ya watu wanapokuwa katika huzuni, hufikiri kuwa matatizo yao ni makubwa kuliko matatizo yanayowapata watu wengine.  

Baadhi hujikuta wakiwakasirikia walioshindwa kuwaonyesha ushirikiano katika kipindi hicho kigumu. Huwezi kumhukumu mtu kwa kosa la siku moja na kusahau wema wote aliofanya zamani. Usiwe hivyo.

Usifikirie mabaya yanayoendelea katika maisha yako

Kuna baadhi watu wanaanza kutengeneza muhtasari wa mambo mabaya ambayo yamewatokea siku za nyuma. Wengine watasema “ndani ya mwezi tu, nimefukuzwa kazi, nimempoteza mzazi, nimepoteza hiki na kile.” Hayo yote, siyo masuala ya kuanza kufikiria wakati unapokuwa na huzuni.


Soma zaidi


Kama unapitia changamoto hizo, ufanye nini?

Nenda kinyume na hayo yote. Mfano badala ya kujifungia ndani, unaweza kuchagua kukutana na watu na kuongea nao kwa sababu itakusaidia kuepukana na huzuni.

Pia, unaweza kufikiria mazuri ambayo umeyapata katika maisha yao badala ya mabaya pekee.

Hakuna anayepitia maisha mazuri kila siku. Wanadamu tumeumbiwa changamoto na ndicho kitu ambacho hutufanya kuimarika zaidi na kuwa wakomavu kifikra na kihisia.

Hadi wakati mwingine, wako katika ujenzi wa Taifa.

Enable Notifications OK No thanks