Samsung kuingiza sokoni simu mpya Agosti 2020

July 28, 2020 2:37 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Atakayenunua Note 20 ultra, ategemee mengi ikiwemo kasi zaidi huku pamoja na nafasi ya kutosha kuhifadhi vitu na uwezo mkubwa wa betri. Picha| What Hi-Fi.


  • Simu hiyo itazinduliwa Agosti kwa njia ya mtandao.
  • Fununu za bei ya simu hiyo, ni kuwa inatarajiwa kuuzwa kwa Sh3.67 milioni.
  • Simu hiyo itazinduliwa sambamba na bidhaa zingine tatu tutoka Samsung.

Dar es Salaam. Kampuni ya kutengeneza bidhaa za kielektroniki ya Samsung inatarajia kuingiza sokoni simu toleo la Note 20 sokoni ili kuwapatia wateja bidhaa zinazoendana na mahitaji yao. 

Kampuni hiyo imeacha maswali kwa wadau wake kama toleo hilo litazifunika simu zote zilizoingia sokoni mwaka 2020 zikiwemo za OnePlus 8 na LG velvet.

Samsung itafanya hafla ya uzinduzi wa simu yake ya Samsung Note 20 Ultra (Galaxy Unpacked 2020) Agosti 5 mwaka huu kwa njia ya mtandao ikiwa ni kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Tunafahamu nini kuhusu ujio wa simu mpya ya Note?

Bila shaka unahitaji kufahamu mawili matatu ili kung’amua kama kweli kuna ulazima wa kuanza kuweka noti kwenye kibubu ukijiandaa na manunuzi ya simu hiyo. 

Fununu za kimataifa zinaeleza kuwa simu hiyo ya Samsung S 20 Ultra itatumia mtandao wa 5G ikiungana na simu zingine zilizotoka hivi karibuni zikiwemo za LG V60 ThinQ, Samsung Galaxy S20 Plus na Motorola Edge Plus.

Atakayenunua Note 20 ultra, ategemee mengi ikiwemo kasi zaidi huku pamoja na nafasi ya kutosha kuhifadhi vitu na uwezo mkubwa wa betri.


Zinazohusiana


Zaidi, Ulinzi wa Note 20 Ultra umeimarishwa kwani inatumia teknolojia mpya ya alama (biometrics) na kama ilivyo kwa simu nyingi zinazotengenezwa mwaka huu, simu hiyo ina uwezo wa kutumia chaja isiyokuwa na waya.

Kamera kubwa zaidi kati ya kamera tatu za simu ya Note 20 Ultra inasemekana kuwa na ukubwa wa Megapikseli (MP) 108 ambayo ni kubwa kuliko Note 10 ambayo ina ukuwa wa MP 16 tu.

Uhifadhi wa Note 20 Ulta siyo haba kwani ina uhifadhi wa RAM wenye ukubwa wa GB 12GB RAM huku uhifadhi wake wa kawaida (ROM) ukiwa ni chaguo kati ya GB  256 na GB 512.

                   

Betri la simu hiyo lina uwezo wa mAh 4500 likiwakwenye simu yenye ukubwa wa inch 6.9.

Ifikapo Agosti 5, tutegemee mengi kutoka Samsungikiweomo vitu vya kuvaa na vingine vinavyokunjwa kwani Note 20 Ultra haitozinduliwa pekeyake.

Hata hivyo siku hiyo, kutakuwa na uzinduzi wa simu zingine mbili za Galaxy Fold 2 na Galaxy Watch 3.

Je upo tayari kuinunua Note 20 Ultra ikiwa bei inayotarajiwa ni Sh3.67 milioni kwa simu yenye ukubwa wa uhifadhi wa GB256 na Sh3.95 milioni kwa Note 20 Ultra yenye ukuwa wa uhifadhi wa GB 512?

Enable Notifications OK No thanks