Mbomipa: Fahari ya utalii Nyanda za Juu Kusini Tanzania

August 15, 2019 4:13 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni eneo la usimamizi wa wanyamapori lilipo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. 
  • Limesheheni wanyama mbalimbali wakiwemo tembo na viboko 
  • Ukiwa Mbomipa unaweza kuburudika kwa kupiga picha, kuwinda na kufanya shughuli za utamaduni. 

Dar es Salaam. Huenda bado unawaza eneo utakalolitumia kwa ajili ya mapumziko yako ya mwisho wa mwaka, wewe na familia yako. Usihofu Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi ya asili ya kuvutia  na kupendeza.

Eneo maalum la usimamizi wa wanyama pori la  Mbomipa lilipo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa huenda likawa eneo sahihi kwako kupumzika mwaka huu kwa sababu limesheni vivutio mbalimbali ikiwemo wanyamapori ambao watakupa burudani wakati wa matembezi yako. 

Mbomipa ni miongoni mwa maeneo matano ya usimamizi wa wanyama pori ya Ipole, Ikone, Randileni na Enduimet yenye mandhari nzuri kwa ajili ya shughuli za utalii.

Eneo hilo ni makazi ya wanyama mbalimbali kama tembo, twiga, pundamilia, viboko na wanyama wengine wengi wenye kuvutia kwa watalii. Pia ni sehemu nzuri kwa jili ya makazi ya wanyama wadogo wadogo kama samaki, ndege, wadudu na wanyama waishio majini.


Zinazohusiana:


Unafikaje Mbomipa?

Kwa mujibu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), inachukua saa 1:30 kusafiri kutoka Iringa mjini hadi katika ofisi za Mbomipa zilizopo katika kijiji cha Tungamalenga kwa kutumia barabara ya changarawe. 

Kama unatoka eneo lolote la Tanzania basi, ukifika Iringa mjini itakua rahisi kufika Mbomipa; eneo tulivu lenye mandhari nzuri.  

Baadhi ya ndege wanaopatikana Mbomipa. Picha|Mtandao.

Utarajie kufanya nini?

Kuna shughuli nyingi unazoweza kufanya katika eneo hilo la utalii ikiwemo safari za kupiga picha za matukio, utalii wa kiutamaduni na uwindaji wa wanyama. 

Mbomipa pia ni fursa kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika utoaji huduma za utalii ikiwemo hoteli ili kujipatia kipato na kuajiri Watanzania. 

Enable Notifications OK No thanks