Mataifa 10 yaliyoongoza kuleta watalii wengi Tanzania Oktoba 2022
December 7, 2022 5:16 am ·
Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
- Ni pamoja na Kenya, Ufaransa, Marekani na Burundi.
- Idadi ya watalii walioingia nchini Oktoba 2022 ilikuwa 141,517.
Dar es Salaam. Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu za Oktoba 2022 (High Frequency Data), idadi ya watalii walioingia nchini Oktoba ilikuwa 141,517 ikiongezeka kutoka 133,998 iliyorekodiwa Septemba.
Hilo ni sawa na ongezeko la watalii 7,519 au asilimia 5.6.
Kuongezeka kwa idadi hiyo kumekuja baada ya idadi ya watalii kushuka miezi miwili mfululizo. Julai mwaka huu Tanzania ilirekodi watalii 166,736 na mwezi uliofuata wakapungua hadi 158,049 kabla hawajapungua zaidi hadi 133,998 mwezi Septemba.
NBS imeeleza kuwa Oktoba mwaka huu, Kenya ndiyo iliongoza kuingiza watalii wengi zaidi nchini ikifuatiwa na Ufaransa, Marekani na Burundi.
Latest
19 hours ago
·
Lucy Samson
Sababu Mbowe kugombea tena uenyekiti Chadema
21 hours ago
·
Lucy Samson
Mbowe kugombea tena uenyekiti Chadema
2 days ago
·
Davis Matambo
Majaliwa akabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa mafuriko Hanang
2 days ago
·
Kelvin Makwinya
Viwango vya kubadili fedha za kigeni leo Disemba 20,2024