Hivi ndivyo ninavyotabasamu kwa kila kazi ninayofanya

April 30, 2020 4:10 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Rodgers kitaaluma ni mwandishi wa habari aliyehitimu katika Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (TUDARCO). Picha|Mtandao.


  • Ni kupitita kutafuta furaha katika kila kazi ninayoifanya na kutokuogopa kukosea.
  • Mbali na hivyo, ninatumia mafunzo yangu ya awali kutengeneza maisha yangu ya kila siku.
  • Bado ninajifunza na nitazidi kujifunza kila iwayo siku huku maoni ya watu yakinijenga na siyo kunibomoa.

Dar es Salaam. Kila mara ninapokutana na rafiki mpya huwa anabaki mdomo wazi kila anapogundua majukumu niliyonayo kila siku.

Mara nyingi swali huwa ni “unawezaje kufanya hayo mambo yote na ukabaki salama na mwenye tabasamu na bashasha kila muda?” Hata hivyo, mara myingi baada ya swali hilo kuibuka, huwa ninakosa majibu.

Kwa muda mrefu, nimekuwa nikijiuliza ni vipi ninaweza kufanya mambo yote ninayoyafanya.

Huenda haunifahamu lakini mimi ni mwandishi wa habari ninayefanya kazi na kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Afrika lakini pia ni mwanamuziki ambaye kwa muda wa ziada ninautumia kubuni vitu mbalimbali vikiwemo nguo, kadi za salamu na mengine mengi.

Haijaishia hapo. Ninafanya kazi kama msaidizi binafsi kwa mrembo mmoja hapa mjini na nimuuza juisi huku kuigiza sauti na kufundisha watu kuimba ikiwa ni kati ya majukumu yangu ya ziada.

Ni machache ndiyo, lakini yote haya saa nyingine yanaenda kwenye ratiba ya siku moja. Ni nini kinachonipa nguvu ya kuyafanikisha na kubaki mwenye tabasamu?

  1. Ni vitu ninavyovipeenda

Tangu zamani, nimekuwa nikipenda kuandika na mawasiliano ni kati ya vitu ninavyo vifurahia. Hivyo kufanya kazi na Nukta habari (www.nukta.co.tz) haijawa safari ngumu bali safari ya kuboresha kile ninachopenda.

Hivyo ni kusema, kama unafanya kitu ambacho unakifurahia, kujifunza kila siku na kujiboresha haitakuwa mateso kwako.

  1. Ninafurahia maoni ya watu juu ya kazi yangu

Tangu ningali mdogo, nimefundishwa “kufanya manuva” nyumbani ikiwemo kutengeneza sharubati ambayo niilikuwa nikikosolewa sukari kuzidi au uchachu kushamiri.

Hilo limenijenga kujifunza kila siku kwenye kazi ninayoifanya na kukubali maoni ninayopewa na kuyafanyia kazi na hivyo kuwa bora kila siku.

Nakumbuka kipindi nimetengeneza sharubati yangu ya kwanza, mmoja wa wadau wangu aliifurahia na hiyo ilikua siku ambayo ilinipatia nguvu ya kuendelea kutengeneza na kuwauzia watu wengi.


Zinazohusiana


  1. Kukubaliana na udhaifu nilionao na kujifunza kutokana na makosa

Watu wengi huogopa kufanya makosa kwa vitu ambavyo huenda wanaviweza lakini hawafahamu kama wanaweza. Utawezaje kufanya hivyo bila kujaribu na kukosea ili ujifunze?

Nikiwa chuoni mwaka wa tatu, nilijitolea kuandika kwenye jarida la kidini na ndipo nilikutana na mwanadada ambaye ninahifadhi jina lake kwa sasa. Mara baada ya kufanya mahojiano naye, niliendelea kuwasiliana naye kumjulia hali hapa na pale. 

Siku moja alinipigia simu na kuniuliza kama ninaweza kufanya maombi ya moja ya tuzo alizoshinda bila uelewa wowote wa kazi hiyo nikakubali na ndicho kilichonipelekea kuwa msaidizi wake binafsi.

 Amekuwa ni rafiki tangu siku hiyo kwa sababu sikuogopa kukosea na kujaribu. Na yeye amekuwa mtu muhimu wa kunifundisha utendaji wa kazi.

Rodgers pia ni mwanamuziki ambaye amekuwa akitumbuiza katika kumbi mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha|Rodgers George.

  1. Ninatafuta furaha katika kila ninachokifanya

Shangazi yangu aliwahi kuniambia,”kama hautabasamu ukiwa unafanya kazi zako, haina haja ya kuendelea kuzifanya”. Ilikuwa baada ya kumlalamikia nilipoanza kuandika habari kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu nilizoea kuandika kwa Kiingereza.

Inachekesha lakini aliongezea kwa kusema “Hakuna kisicho na changamoto”. Huenda shangazi hakumbuki hata muda huo lakini ni jambo ambalo limekuwa likinisaidia kila siku.

Iwe kwenye kuamka saa 10 alfajiri kutengeneza kwa ajili ya wateja wangu, kuimba kwenye majukwaa bila mpunga wowote na hata kuandika makala hii, bado ninafurahia.

Hayo ni mambo amabayo yamekuwa yakinisukuma na kunifanya nifanye kazi zenye makosa hata zile zinazovutia mbele ya watu. 

Kukuta tabasamu kwenye uso wangu siyo kitu kigeni kwani hakuna ninachokifanya bila kukifurahia. Nitafurahi kama na wewe utazidi kufanikiwa kwa kufanya kile upendacho.

Enable Notifications OK No thanks