Hii ndiyo safari unayoweza kuifanya ndani ya chumba chako

Rodgers George 0805Hrs   Aprili 20, 2020 Safari
  • Unaweza kusikiliza “Podcasts” au kusoma vitabu vya safari na kufahamu mambo mengi usiyoyajua.
  • Kwa kufanya hivyo, utaepukana na kurudia ratiba yako na kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii.
  • Hautatalii peke yako bali utajifunza na kuelimika kwa gharama nafuu yaani bila haja ya kupaki begi lako.

Dar es Salaam. Kama unapenda kusafiri, hauna haja ya kubadili mikao kuanzia asubuhi hadi jioni kwenye kochi lako na kuhamia kwenye kitanda. Simu yako inaweza kukupeleka kokote kule duniani.

Umewahi jiuliza kuwa kwa kutumia bando lako la intaneti mambo yanaweza kwenda unavyotaka ikiwemo kusafiri kwa njia ya mtandao kutakuongezea manufaa zaidi kuliko kukesha kwenye mitandao ya kijamii?

Kama unaungana na hilo, Nukta (www.nukta.co.tz) imekuletea njia za wewe kusafiri huku ukiwa chumbani kwako.

1. Kutazama filamu za safari

Unaweza kudhani ni mzaha lakini kupitia filamu hizi unaweza kugundua hata ambayo haujawahi kuyagundua.

Tovuti ya wadau wa safari ya The guardian imeorodhesha filamu hizo zikiwemo “Real-Life Adventures” ya mwaka 2014, “Tracks” ya mwaka 2013 na zinginezo nyingi zinazopatikana kwenye tovuti na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni yakiwemo ya Netflix, Google Play na Amazon.

Filamu ya Lion ya mwaka 2016 ni kati ya filamu zinazoweza kukupeleka maeneo ambayo hata ndoto zako hazijawahi kuota. Picha| Kobal/REX/Shutterstock.

2. Tembelea hifadhi za wanyama

Zipo hifadhi ambazo zina hadi mtu wa kukuelezea mtandaoni ambaye atakupatia safari hiyo yote kwa gharama za bando lako la intaneti tu.

Hifadhi mbalimbali za nje ya nchi sasa zinakupatia nafasi ya kuzitembelea kidijitali. 

Hifadhi hizo ni pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Huwai’i Volcanoes ya nchini marekani ambayo ni kati ya hifadhi inayotumia teknolojia ya nyuzi 360 kutengeneza utalii huo unaokupatia hadi mfumo wa sauti kusikia milio ya ndege na kufanya yasiyowezekana ikiwemo kuruka juu ya mlima ukiwa umekaa kwenye kochi lako.

3. Sikiliza “Podcast” za safari

Kwa mujibu wa kamusi ya Oxford, podcast ni sauti iliyowekwa kwenye intaneti na inaweza kupakuliwa kwenye simu au kompyuta. Mara nyingi ipo kwenye mfumo wa mazungumzo.

Tovuti ya Travel Noire imeorodhesha “Podcast” zaidi ya tano zikiwemo “Vacation Mavens” iliyoandaliwa na Kimber Tate na Tamara Gruber. Hauhitaji kurudia orodha ya nyimbo zako siku nzima, safiri kwa mfumo wa sauti.


Zinazohusiana


4. Soma kitabu cha safari

Huenda unapenda kusoma vitabu na kusafiri vilevile. Lakini inakuwaje ukifahamu kuwa unaweza kusafiri kwa kusoma vitabu? Ndiyo, vuta kitabu chako na safiri bila haja ya kukata tiketi wala kufungasha begi lako.

Jarida la Forbes limeorodhesha vitabu vikiwemo  “The Rings of Saturn” kilichoandikwa na W.G. Sebald na “A Moveable Feast (Life Changing Food Adventures Around The World)” kilichohaririwa na Don George.

Bado utaendelea kurudia “playlist” yako kwa siku nzima? Tenga muda na usafiri kwa gharama ya bando lako.

Related Post