Hifadhi ya taifa Mto Ugalla, mahali pa kushuhudia mwanzo wa maisha mapya

January 27, 2020 10:26 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pepo inayochukua zaidi ya kilometa za mraba 3000 za ardhi ya kitanzania.
  • Inavivutio vingi vikiwemo Mto Ugalla ulio mashariki mwa Ziwa Tanganyika.
  • Ni kati ya vivutio vichache unavyoweza kufurahia kuvuna asali pia.

Dar es Salaam.Ukanda wa mashariki wa Ziwa Tanganyika, kuna mto ubebao maisha ya mamia ya viumbe hai ambao unakatiza  kwa madaha huku ukivutia viumbe kadha wa kadha kwenye hifadhi ya Mto Ugalla ambao ni kati ya hifadhi  mpya za taifa.

Ndiyo, mto huo ambao unanywesha maelfu ya wanyama wakaao kwenye hifadhi ya taifa ya Mto Ugalla ni kati ya mito yenye kuendelea kuifanya nchi ya Tanzania kuwa moja wapo ya pepo kwa wanayama pori na hata viumbe wengine adimu.

Hifadhi hiyo ambayo historia yake inaanzia mwaka 1965 ni hifadhi ya Taifa ambayo imepata cheo hicho mwaka 2019 na kuifanya kuwa ardhi yenye ukubwa wa kilometa za mraba 3,865 na yenye vivutio vya kipekee kati ya hifadhi za Tanzania.

Huenda unajiuliza ni nini kipya kwani wanyama waliopo kwenye hifadhi hii wapo kila kona ya nchi lakini pepo hii ya Mto Ugalla ni kati ya hifadhi chache unazoweza kuvuna asali.

Ndiyo, Asali ambayo ni kimiminika chenye upekee wake ni kati ya vivutio ambavyo ni mbali na uvuvi ambavyo utavipata kwenye ardhi hii ya Kitanzania.

Kama umezowea kuona ng’ombe na mbuzi pekee wakiongeza kiumbe hai duniani, unaweza kubadirisha mazowea yako kwa kuona jinsi gani swala na wanyama pori wengine huongeza idadi yao duniani uwapo kwenye mchanga ang’avu wa ardhi hii.


Zinazohusiana


Utaenda lini?

Sio mbaya kutembelea hifadhi hii kwenye msimu wa mvua kama wewe mapenzi yako yapo kwenye kutazama ndege lakini, unaweza kupata changamoto ya barabara kutokana na mvua kali zinazonyesha kwanzia mwezi Januari hadi Aprili.

Kama wewe mapenzi yako ni kwa wanyama wengine tofauti na ndege kama southern ground hornbill na Shoebill, kipindi cha ukame ni kipindi mahsusi kwaajili yako kuona wanyama nadra wanaotembelea Mto Ugalla kukata kiu.

Wanyama hao ni pamoja na Topi na Roan ambao hautawapata kwenye bara lingine isipokuwa Africa huku ukifurahia hali ya hewa yenye sentigredi 13 hadi 41 kwenye ardhi hii yenye upekee duniani.

Unasubiri nini kuchukua kofia yako, miwani na darubini kuanza safari yako ya kutalii kwenye pepo hii iliyosheheni maajabu mengi ya Kiafrika?

Wanyama hao ni pamoja na Topi na Roan ambao hautawapata kwenye bara lingine isipokuwa Africa huku ukifurahia hali ya hewa yenye sentigredi 13 hadi 41 kwenye ardhi hii yenye upekee duniani. Picha| Pinterest.

Enable Notifications OK No thanks