Google yatoa ahueni kwa wanunuzi wa bidhaa mtandaoni

August 17, 2019 6:15 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inawawezesha kununua programu za simu bila kuwa na neno la siri la akaunti ya Google. 
  • Mnunuzi anaweza kutumia neno la siri, alama za vidole au “pattern” za kuingilia kwenye simu yake. 
  • Baadhi ya wadau wamesema mabadiliko hayo yanaweza kuleta changamoto ya usalama. 

Dar es Salaam. Kampuni ya Google imeanzisha utaratibu mpya unaowawezesha watumiaji wa bidhaa zake kununua programu mbalimbali bila kuhitaji kuwa neno la siri (Password) ya akaunti ya Google. 

Kwa sasa mnunuzi wa bidhaa hizo za mtandaoni anaweza kutumia mfumo wa usalama wa kuingilia simu yake (Sim lock). 

Anaweza kutumia alama za vidole “fingerprint”, neno la siri, “Face id” na hata “pattern”kufanya manunuzi ya programu tumishi za Google na hata zinazotumiwa na simu. 

Mbadiliko hayo yatawasaidia watu waliosahu au kupoteza neno la siri wanalotumia kuingilia katika akaunti za Google na hivyo kufanya manunuzi wakati wowote. 

Hata hivyo, neema hiyo siyo kwa watumiaji wote wa simu kwani inawahusu watumiaji wa simu zinazotumia mfumo endeshi wa “Android 7” tu zikiwemo simu za Samsung S8 na Sony Experia XZ.

Hadi sasa, baadhi ya simu zinazotumia mfumo endeshi wa “Android” zina uwezo wa kufanya manunuzi ya apps kwa kutumia teknolojia ya alama za vidole na kuingia kwenye programu tumishi mbalimbali.


Zinazohusiana


Kitu ambacho ni kipya, kwa sasa watumiaji wa simu hizo wanaweza kuingia kwenye programu za Google bila kuandika neno la siri kama ilivyokua hapo awali.

Hata hivyo, Google bado inaendelea kuingiza teknolojia hiyo kwenye orodha ya huduma zake lakini kwa wakati huu mtu anahitaji kutembelea huduma za ulinzi za Google ili kuunganishwa.

Wadau wa teknolojia wameaimbia www.nukta.co.tz kuwa mabadiliko hayo ambayo Google inakusudia kuyafanya yanaweza kuongeza matishio ya usalama binafsi kwani taarifa za alama za vidole zinakua zimezagaa mtandaoni.

Mike Roosevelt ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesomea masuala ya teknolojia ya mawasiliano “IT” amesema mabadiliko hayo yana faida na hasara.

“Ni vizuri kwani mtu hahitaji kukumbuka neno lake la siri na hata kama akipoteza simu yake basi mhalifu hawezi kubashiri neno lake la siri,” amesema Mike

Kwa upande wa hasara, Mike amesema haoni kama ni salama kwa taarifa za alama za vidole kutumika kwenye mitandao kwani wadukuzi ni wengi hivyo wanaweza kuzitumia kuzifikia taarifa za watu ambazo ni siri. 

Enable Notifications OK No thanks