Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki dunia

June 9, 2020 2:33 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amefariki dunia baada ya kukumbwa na shambulio la moyo ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais mteule Evariste Ndayishimiye.

Dar es Salaam. Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki dunia baada ya kukumbwa na shambulio la moyo ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais mteule Evariste Ndayishimiye.

Nkurunziza aliyeiongoza Burundi kwa miaka 15, amefikwa na umauti Jumanne (Juni 9, 2020) katika hospitali ya kumbukumbu ya 50 ya Karusi—Mashariki ya kati ya Burundi–baada ya kulazwa kutokana maradhi ya moyo Juni 8, taarifa ya Serikali iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter imeeleza.

Kiongozi huyo amefariki ikiwa ni takriban wiki tatu tu baada ya nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki kukamilisha uchaguzi mkuu ulioshuhudia jenerali wa zamani wa jeshi Ndeyishimiye akishinda kwa asilimia 68.7 ya kura zote.


Soma zaidi:


Ndayishimiye aliteuliwa na chama tawala nchini humo cha CNDD-FDD kuwania nafasi hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wagombea wengine saba katika uchaguzi uliofanyika Mei 20.

Nkurunziza (55) alikuwa akitarajiwa kukabidhi madaraka hayo kwa kiongozi huyo mpya mwishoni mwa Agosti 2020 baada ya kukamilisha kipindi chake cha uongozi.

Kipindi cha mwisho cha utawala wa Nkurunziza kilitawaliwa na mivutano ya ndani ikiwa ni tofauti na siku za awali alipotwaa madaraka hayo mwaka 2005.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV