Rais Samia: Vyombo vya usalama viongeze kasi, juhudi za uokoaji waliofukiwa na kifusi Shinyanga

August 14, 2025 5:57 pm · Esau Ng'umbi
Share
Tweet
Copy Link

Rais wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kupeleka misaada ya dharura na kuongeza juhudi za uokoaji kwa wachimbaji wa madini waliofunikwa na kifusi mkoani Shinyanga.

Agizo hilo limekuja mara baada ya mashimo matatu katika mgodi wa Nyandolwa, Kata ya Mwenge, Wilaya ya Shinyanga Vijijini kufunikwa na kifusi baada kutitia yakiwa na wachimbaji 25 ndani yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mohamed Mhita idadi ya wachimbaji waliokuwa katika mashimo hayo ni 25, ambapo shimo la kwanza lilikuwa na wachimbaji 11, shimo la pili lilikuwa na wachimbaji 8, na shimo la tatu lilikuwa na wachimbaji 6. 

Kati ya hao wanne waliokolewa lakini mmoja aliyeokolewa alifariki dunia baadaye.

Aidha, Rais ametoa pole kwa ndugu, jamaa, na Watanzania wote walioguswa na maafa hayo, akisisitiza mshikamano na msaada kwa familia, zilizoathirika.

“Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu awajalie pona ya haraka majeruhi, na pia awape subra na nguvu ndugu, jamaa na marafiki wa wale wote walioathiriwa na maafa haya,” amesema Rais Samia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV