Rais Samia: Tutaajiri watumishi wa afya uchumi ukikua

October 16, 2021 10:48 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema Serikali huongeza ajira za watumishi kulingana na ukuaji wa uchumi wa Taifa.
  • Asema utoaji ajira huzingatia kada muhimu ikiwemo ya afya na elimu.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatumia vigezo mbalimbali kutoa ajira za watumishi wa afya ikiwemo ukuaji wa uchumi wa Taifa na haiwezi kuvuka vigezo hivyo ili kuepuka changamoto za ulipaji wa mishahara.

Hata hivyo, amekiri kuwa vituo vya afya na hospitali bado vinakabiliwa nauhaba wa watumishi na Serikali itaendelea kuajiri kulingana na ukuaji wa uchumi. 

“Uhaba wa watumishi si kwa KCMC peke yake. Tunakabiliwa na uhaba wa watumishi kwenye mahospitali yetu yote na hii ni kutokana na ukuaji wa kiwango cha uchumi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia alikuwa akizungumza leo (Oktoba 16, 2021) katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Kiongozi huyo mkuu wa nchi amesema ulipaji wa mishahara ya watumishi wa Serikali inategemea ukuaji wa uchumi na haiwezi kuajiri watumishi wapya ikiwa uchumi hauruhusu. 

“Kila tunapopata upenyo, uchumi ukikua kidogo, tunafanya ajira haraka haraka hasa hizi zinazogusa maisha ya wananchi; madaktari, wauguzi lakini waalimu pia,” amesema a Rais Samia.

Hata hivyo, KCMC ambayo haijapata  watumishi kwa miaka minne iliyopita, Rais Samia amesema Serikali itakapopata “upenyo” wa kuajiri na uchumi ukukua, hospitali hiyo itakuwa na sehemu fungu lake la watumishi wa afya katika maeneo muhimu.

Pamoja na hayo, Rais Samia amewasisitizia wananchi wa Kilimanjaro kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona ambao bado upo nchini.

Februari 10, 2021 akiwa bungeni, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dk Godwin Mollel alisema sekta ya afya nchini ina upungufu wa watumishi 16,000.

Hata hivyo, alisema katika mwaka wa fedha wa 2021/22, sekta ya afya inatarajia kuajiri watumishi wapya 12,476.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV