Rais Samia ateua wanne kuwa wenyeviti wa bodi

February 11, 2026 5:42 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Walioteuliwa ni pamoja na Makinda, Dk Chuwa, Machano na Prof Maboko.

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa vigogo wanne kuwa wenyeviti wa bodi mbalimbali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo Februari 11, 2026 inabainisha kuwa Anne Samamba Makinda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Makinda aliyewahi kuwa kushika nyadhifa kubwa nchini Tanzania ikiwemo Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015 ameteuliwa katika nafasi hiyo baada ya kuhudumu katika nafasi ya kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Wengine ni Jaffer Machano aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) akichukua nafasi ya Ally Amani Karavina.

Aidha, Rais Samia pia amemteua Dk Albina Andrew Chuwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) na Prof Makenya Abraham Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV