Rais Samia asisitiza kudumisha usalama, umoja, amani nchini

August 22, 2023 3:30 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema haitawezekana kuligawa/kuuza au kuharibu amani yaTaifa.
  • Askofu Shoo amtaka aendelee kutumia hekima kufanya maamuzi.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendelea kudumisha usalama, umoja, na amani kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na kuongeza kuwa kamwe haitawezekana kwa mtu au kikundi cha watu kuligawa Taifa.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) leo Agosti 21, amewaambia wahudhuriaji kuwa amekuwa akikaa kimya hata pale anaposikia kauli za maudhi na ataendelea kukaa kimya.

“Niliamua kunyamaza kimya na naendelea kunyamaza kimya, ninachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili, wa kuuza taifa hili, wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye taifa hili, huu ndio ujumbe wangu kwenu,” amesema Rais Samia jijini Arusha.

Ujumbe huo wa Rais Samia, unatokana na hotuba ya Askofu Mkuu wa kanisa la KKKT Dk.Fredrick Shoo aliyemuomba Rais Samia kutumia hekima katika kukabiliana na ukosoaji wa mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai unaoendelea.


Soma zaidi


Itakumbukwa tangu Bunge la Tanzania lilipopitisha azimio la ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai, makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wanasheria pamoja na wanaharakati yamekuwa yakiibuka kuukosoa mkataba huo huku wengine wakitaka ufutwe kabisa.

Hata hivyo, Dk. Shoo amebainisha kuwa wao kama viongozi wa dini walishakutana na Rais na kumweleza mapungufu ya kufanyiwa kazi kwenye mkataba huo ambapo Rais Samia aliahidi kuyafanyia kazi.

“Sisi viongozi wa dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona mwanzoni kabisa mwa jambo hili na ulitupokea, ukatusikiliza maoni yetu na ukaahidi maoni hayo utawapa wataalamu wayafanyie kazi kwa uzito unaostahili kwa maslahi mapana ya Taifa,” amesema Dk. Shoo.

Aidha, Rais Samia ametumia maadhimisho hayo kusisitiza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuyatumia kama fursa kupitia kilimo cha umwagiliaji ili kuzalisha mazao kwa wingi yatakayosaidia kuimarisha usalama wa chakula.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV