Rais Samia aomboleza kifo cha Rais Lungu

June 6, 2025 12:07 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Edgar Lungu akumbukwa kwa uongozi wa amani, maendeleo ya miundombinu.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kilichotokea nchini Afrika Kusini, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, Rais Samia amesema amesikitishwa na taarifa hizo za msiba.

“ Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi za dhati kwa Mheshimiwa Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia, familia ya Rais Lungu, marafiki zake na wananchi wote wa Zambia. Roho yake ipumzike kwa amani,” inaeleza taarifa hiyo.

Rais Edgar Lungu ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 68. Picha/ Alton Telegraph.

Edgar Chagwa Lungu alikuwa Rais wa sita wa Zambia kati ya mwaka 2015 hadi 2021, baada ya kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Michael Sata aliyefariki dunia akiwa madarakani. 

Baada ya kushindwa uchaguzi wa 2021 na Rais Hakainde Hichilema,  Lungu alistaafu siasa lakini alirejea mwaka 2023 kama mgombea wa upinzani. 

Hata hivyo, Desemba 2024 Mahakama ya Katiba ilimtangaza kuwa hastahili kugombea tena urais.

Kwa Wazambia na watu wa Afrika, Edgar Lungu atakumbukwa si tu kwa mchango wake wa kisiasa, bali pia kwa imani yake thabiti, utulivu wake, na dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa lake.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV