Rais Samia amteua Mobhare Matinyi kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali

October 2, 2023 5:09 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Anachukua nafasi ya Gerson Msigwa iliyokuwa wazi kwa siku nane.
  • Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa muda wa siku 91.

Dar es Salaam. Baada ya kutokuwa na msemaji mkuu wa Serikali kwa takriban siku nane, hatimaye, Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo ambaye pia atakuwa msemaji mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu usiku wa leo Oktoba 2, 2023 imebainisha kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.

Mobhare Matinyi ni mwanahabari mkongwe na mahiri. Aliwahi kuwa Mhariri wa gazeti la Majira, amekuwa akifundisha diplomasia na mtaalamu wa mawasiliano kwa umma.

Matinyi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam anaenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa ambaye Septemba 23, 2023 aliteuliwa na Rais Samia kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Said Othman Yakubu ambaye aliteuliwa kuwa balozi.

Uteuzi wa Matinyi unazima minong’ono ya chini kwa chini iliyokuwa ikiwahusisha baadhi wa waandishi wa habari wakongwe nchini Tanzania kushika nafasi hiyo.


Soma zaidi : Rais Samia apangua vigogo TTCL, Tanesco, vilio vya umeme vikiendelea Tanzania


Matinyi amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa muda wa siku 91 pekee ambapo aliteuliwa Julai 2, 2023 akichukua nafasi ya Mwanahamisi Nkunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Uteuzi huo unafanya mpaka sasa kuwe na nafasi mbili za ukuu wa wilaya zilizoachwa wazi ikiwemo ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo ambaye jana Octoba Mosi, 2023 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilimteua kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV