Rais Samia akutana na mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza

November 1, 2021 6:34 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza, Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland Oktoba 31, 2021. Picha| Ikulu.


  • Wakutana kuzungumzia masuala ya biashara kati ya nchi hizo mbili.
  • Mjumbe huyo akiahidi kushawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza Tanzania.

Dar es salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumza na mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Lord John Walney kuhusu masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania.

Rais Samia amekutana na Walney Oktoba 31, 2021 kando ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira (CO26) Glasgow,Scotland kwa lengo la kujitambulisha huku akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili katika masuala ya biashara na utalii.

Mjumbe huyo ameweka bayana kuwa kukutana kwake na Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamuwezesha kuwashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya biashara na utalii Tanzania.

Rais Samia ameeleza kuwa Serikali yake ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuboresha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi kati ya Tanzania na Uingereza.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV