Rais mteule Ruto atoa mwelekeo wa serikali yake siku 100 za mwanzo

September 5, 2022 2:01 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Kupambana na ufisadi na rushwa.
  • Pia kukuza uchumi na kushirikiana na wapinzani wake. 

Dar es Salaam. Baada ya Mahakama Juu Nchini Kenya kubariki William Ruto kuwa rais wa nchini hiyo, ameahidi kukuza uchumi, kushirikiana na wapinzani na kupambana na rushwa ndani ya 100 za uongozi wake.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jioni ya Septemba 5, 2022, Rais Ruto amemshukuru Mungu na kuwapongeza Wakenya waliojitokeza kumpigia kura na kwamba ni faida kwa watoto wao pia kupata nafasi za uongozi.

Ruto ameipongeza Mahakama ya Juu kwa maauzi iliyofikia sambamba na kumpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati kwa kumuita “shujaa” katika uchaguzi wa mwaka huu.

Ahadi zake wa Wakenya

Kuhusu kukuza uchumi Rais mteule Ruto amesema kuwa wanajipanga kukamilisha miradi iliyokuwa ikiendelea na kufungua miradi mipya siku za usoni itakayohakikisha upatikanaji wa mbolea, kuongeza thamani za bidhaa na ujenzi wa makazi pindi watakapoingia ofisini.

Ameahidi pia kupambana na ufisadi kwa kuanzisha mfuko wa mahakama utakaoipa uhuru wa kufanya kazi bila ya kuitegemea serikali kuu.

Katika mkutano huo amewapongeza wagombea wenzake wa vyama pinzani huku akisema atazungumza na Raila Odinga ambaye amemtaja kuwa “mshindani wake anayestahili” na kujadili masuala ya jinsi watakavyofanya kazi pamoja kama mpinzani.

“Ili tuanze kuweka muktadha jinsi tutakavyofanya kazi pamoja kwa ajili ya watu wa Kenya. sisi ambao tutafanya kazi katika timu ya watendaji na Azimio katika upinzani,” amesema.

Pia amesema hachukizwi na uamuzi wa Raisi Uhuru aliyemaliza muda wake kuunga mkono hasimu wake wa kisiasa, Raila Odinga, na kwamba licha ya kutowasiliana nae kwa kipindi kirefu atampigia simu kuhusu mchakato wa mpito.

“Hivi karibuni nitampigia simu Rais Uhuru Kenyatta. Sijazungumza naye kwa miezi kadhaa. Tutakuwa na mazungumzo kuhusu mchakato wa mpito. Tutasalia kuwa marafiki,” amesema na kuahidi kumpa Uhuru heshima anayostahili anapoelekea kustaafu.

Kwenye mkutano huo, Ruto alipuuzilia mbali mipango yoyote ya “kupeana mkono” na Odinga kama mtangulizi wake alivyofanya.

“Ninaamini katika utawala wa sheria, siamini katika hadithi za kupeana mikono,” amesema. “ninaamini katika Serikali inayowajibika inayowajibishwa na upinzani unaowajibika.”

Hata hivyo Ruto ameahidi kumpa heshima inayostahili Odinga wakati atakapoamua kustaafu masuala ya siasa “rafiki yetu wa dhati Raila Odinga atakapostaafu, pia tutampa heshima anayostahili kama kiongozi wa Kenya ambaye ametoa mchango mkubwa kwa demokrasia ya taifa letu,” amesema Ruto.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV