Polisi Tanzania yakiri kumshikilia Mwanahabari Kabendera

July 30, 2019 11:05 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Mwanahabari, Erick Kabendera aliyedaiwa kutoweka hakutekwa bali alikamatwa na polisi na anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu uraia wake.

Mambosasa aliyekuwa akizungumza na Wanahabari leo (Julai 30, 2019) amesema walimkamata Kabendera jana jumatatu nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam baada ya kukaidi wito wa kufika polisi.  

“Aidha mwandishi huyo awali aliandikiwa barua ya wito kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi wito huo.

“Baada ya kukamatwa mwandishi huyo tumesikia taarifa mbalimbali zikisambaa kuwa mwandishi huyo ametekwa, niseme kuwa mwandishi huyo hajatekwa ila tumemkamata kwa mahojiano,” amesema Mambosasa. 

Amesema wanamshikilia na wanaendelea kuwasiliana na maofisa wa Uhamiaji ili Mwanahabari huyo ambaye anafanya kazi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi ahojiwe kutokana na mashaka kuhusu uraia wake. 

“Aidha mtuhumiwa huyo kuna mashaka makubwa kuhusiana na uraia wake tutakapobaini mara moja tutamkabidhi kwenye Idara ya Uhamiaji ili kushughulika naye na ndiyo maana alikuwa akikaidi wito wa polisi na kujihami kuwa ametekwa,” amesema.


Soma zaidi: 


Katika hatua nyingine, Mambosasa amewataka wananchi kutii sheria za nchi bila shuruti ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. 

Wakati Kabendera akishikiliwa na Polisi, watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Twitter wameendelea kupaza sauti zao ili kushinikiza kupatikana kwa Mwanahabari Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi ambaye alitoweka tangu Novemba 21, 2017 na hajulikani alipo  mpaka leo 

Gwanda ni mmoja wa waaandishi waliokuwa wanaripoti juu ya mfululizo wa mauaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Namna uhaba wa nyani, pofu unavyohatarisha ndoa za Wahadzabe

Namna uhaba wa nyani, pofu unavyohatarisha ndoa za Wahadzabe

Nukta TV

Hii ndio mikoa yenye watu wenye kipato kikubwa zaidi Tanzania

Hii ndio mikoa yenye watu wenye kipato kikubwa zaidi Tanzania

Nukta TV

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Nukta TV