Polisi kuimarisha ulinzi sikukuu ya Eid

May 2, 2022 12:29 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Lawahakikishia waumini wa dini ya Kiislamu utulivu na amani wakati kisheherekea siku hiyo.

Mwanza. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga vyema katika kuhakikisha sherehe za sikukuu ya Eid al-Fitr zinasheherekewa kwa amani na utulivu.

Taarifa ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi kwa vyombo vya Habari leo Mei 2, 2022 imesema ulinzi utaimarishwa kwenye nyumba za ibada ambapo askari watakua wakipita kwa doria za miguu, pikipiki na magari katika maeneo yote ya Jiji na Mkoa wa Mwanza.

Kamanda amewataka wananchi wanapokwenda kwenye nyumba za ibada au kumbi za starehe wasiache nyumba zao bila uangalizi au kuziacha wazi kwani kunaweza kushawishi wezi kuiba.

Kamanda Ng’anzi amewakumbusha wazazi na walezi kuwa pamoja na kusherekea sikukuu hii wasisahau majukumu yao ya kuwa makini na watoto wao kwa kutowaacha peke yao barabarani na katika sehemu za michezo mfano maeneo ya mialo na kwenye bembea.

“Katika sherehe hizo polisi tunapiga marufuku disko toto, vile vile ni marufuku kwa madereva wa vyombo vya moto kuendesha wakiwa wamelewa au mwendo kasi, endapo ikibainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” amesema Kamanda Ng’anzi

Sikukuu ya Eid al-Fitr kwa Tanzania itasheherekewa kesho, huku nchi nyingine ikiwemo Kenya zinasheherekea leo.

Ofisi za Mufti wa Tanzania na Zanzibar zilitoa taarifa jana na kutangaza kuwa mwezi haukuandama, hivyo Sikukuu ya Eid al-Fitr itakuwa Mei 3, 2022.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV