Njia mbadala za kupika mboga kwa kutumia mvuke

March 21, 2022 5:01 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Unahitaji sufuria kubwa, chujio na bakuli.
  • Kwa mbogamboga, utahitaji hadi dakika 15 kuivisha.

Huenda unadhani unahitaji sufuria maalumu ili upike mboga na chakula chako kwa kutumia mvuke.

Hapana, wakati mwingine vyombo vya nyumbani vinatosha kabisa kukuwezesha upike mboga zako za majani kwa njia ya mvuke.

Mahitaji

1: Sufuria kubwa.

2: Bakuli lenye kitako kipana.

3: Chujio la bati lisilo na mshikio au chuujio la nazi.

4: Mfuniko unaotosha vizuri kwenye sufuria.

Kazi ianze

Weka maji kwenye sufuria na kisha bandika sufuria jikoni. Kalisha bakuli ndani ya maji hayo na ni vyema bakuli likawa katikati ya sufuria.

Washa moto ili kuruhusu maji yachemke na kisha anza kuandaa mboga yako.

Kwa mboga za majani ambazo zinahitaji chumvi unaweza kutumia njia ya sufuria ndani ya sufuria. Yaani badala ya chujio, tumia sufuria.

Licha ya kuwepo sufuria maalumu za kupika kwa mvuke, unaweza kutumia njia zingine. Picha| Better homes and gardens.

Maji yakichemka, weka mboga unayotaka kupika kwenye chujio na kisha ukalishe chujio hilo kwenye bakuli ndani ya sufuria.

Funika sufuria na unaweza kuweka kitu kizito juu ya mfuniko ili kutokuruhusu kabisa mvuke utoke. 

Kwa njia hii mboga za majani zinahitaji dakika 10 hadi dakika 15. Baada ya hapo funua sufuria na utoe mboga zako. Unaweza kuwa unageuza mara moja moja wakati ukisubiri.

Utake nini tena? JikoPoint ndiyo mambo yote.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Nukta TV

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Nukta TV