Namna ya kuandaa kachori za mbogamboga

December 2, 2024 4:03 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Unaweza kutumia kabichi au mboga uipendayo.
  • Kachori huupa mwili virutubishi vingi. 
  • Unaweza kutumia kachori hizi na juisi, soda ama chai.

Je umeshawahi kula kachori za mbogamboga? Kama bado leo nitakupa maujanja. 

Baadhi ya watu wamezoea kachori lazima ziwe zimepikwa kwa viazi mviringo (viazi mbatata), mihogo au viazi vitamu jambo ambalo limekuwa ni kawaida katika jamii za Afrika.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) utumiaji wa mbogamboga katika kila mlo husaidia kuzuia na kukabiliana na saratani na kuimarisha mfumo wa kingamwili na kukuepusha na magonjwa.

Hivyo leo ndani ya jikopoint.co.tz unajifunza njia mpya ya kupika kachori kwa kutumia mchanganyiko wa mbogamboga ambazo sio tu zina ladha tofauti lakini pia zina faida nyingi kiafya.

Hatua kwa hatua namna ya kuandaa

Hatua ya kwanza, chukua karoti, hoho, kabichi na vitunguu safisha kwa maji safi ili kuondoa uchafu na wadudu. Kisha zimenye na kuzikata katika vipande vyembamba na virefu. Pia katakaka kabichi. 

Baada ya hapo weka maji motoni katika sufuria yako na yaache yachemke kwa dakika 3 kisha weka mchanganyiko huo hapo juu na uongeze chumvi kiasi.

Geuza kwa dakika 2 usiache vichemke kwa muda mrefu. Baada ya hapo epua kutoka katika sufuri lenye maji ya moto kiasi na uwekwe kwenye chombo chenye maji ya baridi kwa lengo la kupoza mboga mboga.

Mboga ikipoa chuja kwa chujio ili kuondoa maji katika mchanganyiko wako. Katika bakuli lingine weka unga wa ngano robo kilo,  pilipili (kama unapenda ila sio lazima), majani ya kotimiri kiasi kisha ongeza mbogamboga na uchanganye mchanganyiko huo mpaka ushikane vizuri na unga.

Baada ya hapo tengeneza madonge madogo mfano wa mpira. Hatua inayofuata weka mafuta ya kutosha kwenye kikaango. 

Mafuta yakipata moto, weka kachori moja baada ya nyingine na kaanga mpaka ziwe na rangi inayovutia. Hakikisha moto usiwe mkali sana ili ziive vizuri. 

Kufikia hatua hiyo kachori zako za mboga mboga  zitakuwa tayari kwa kuliwa na unaweza kula na juisi, soda, chai ama zenyewe ni wewe tu upendavyo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV