Ni uzushi: Chanjo ya corona haina virusi vya Ukimwi

July 15, 2020 8:11 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Siyo kweli kuwa chanjo ya Corona ina virusi vya Corona.
  • Ukweli ni kuwa wagonjwa wa Ukimwi wanaweza kupata changamoto ya matibabu wakati huu wa janga la Corona.

Dar es Salaam.Habari za uzushi kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona hazina mipaka. Na sasa chanjo ya COVID-19 imeanza kuzushiwa kuwa ina virusi vya Ukimwi.

Uzushi huo unavumishwa katika kipande cha video inayosamba kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Youtube inayoeleza  kuwa Afrika imegoma kupewa chanjo ya corona inayodhaniwa kuwa ina virusi vya Ukimwi wakati habari hiyo siyo ya kweli.

Video hiyo iliwekwa mtandaoni Julai 6, 2020 ikiwa na maelezo katika lugha ya kiswahili  ikieleza kuwa “Habari hivi punde Afrika yagoma kupewa chanjo ya corona. Chanjo yasadikika kuwa na virusi vya ukimwi.”


Zinazohusiana:


Ukweli ukoje

Timu ya Nukta Fakti imebaini kuwa habari hiyo ni uzushi na haina ukweli wowote.

Ukitazama habari hiyo ambayo ilikuwa ni taarifa ya habari kutoka Indhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC) ilikuwa inaeleza habari mbalimbali ambapo moja ilikuwa inaeleza kuhusu wagonjwa wa Ukimwi wasiofikiwa ipasavyo kutokana na janga la Corona.

Kimsingi habari hiyo haikuelezea kuhusu chanjo ya Corona kuwa na virusi vya Ukimwi. Kwa hiyo inapaswa kupuuzwa.

Enable Notifications OK No thanks