Netflix kuja na mpango mpya kwa watazamaji wa filamu mtandaoni

March 18, 2022 7:29 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Itawawezesha akaunti moja ya jukwaa hilo kutumiwa na watu wengi.
  • Itakuwa inawatoza kiasi fulani cha fedha.
  • Mpango utaisaidia kuongeza mapato ya kila mwaka.

Dar es Salaam. Jukwaa la mtandaoni la filamu la Netflix linaratajia kuanza kufanya majaribio ya kuwatoza pesa watu wanaotumia akaunti moja ya jukwaa hilo ili kuongeza wigo wa mapato na kuimarisha usalama wa watumiaji wake.

Netflix imesema hivi karibuni imegundua ongezeko la watazamaji wa filamu kupitia jukwaa hilo lakini wengi wao wanatumia akaunti zinazofanana, ikimaanisha akaunti moja inatumika na zaidi ya mtu mmoja. 

Uongozi wa jukwaa hilo umesema kwa sasa gharama za utengenezaji maudhui ya video zimepanda, hivyo kuna umuhimu wa kufanya maboresho ya namna watu wanavyotumia jukwaa hilo. 

Siku zijazo, Netflix itaanza kufanya majaribio kwa  kuwapa watumiaji waliojisajili nchini Chile, Costa Rica na Peru chaguo la kuongeza watu kwenye “akaunti ndogo” kwa ada ya kila mwezi ya Dola za Marekani 2 hadi 3 (Sh4,600 had Sh6,900).

Hiyo ina maana kuwa mtu mwenye akaunti anaweza kuwa akaunti nyingine ndogo kwa ajili ya ndugu na marafiki zake lakini atalazimika kulipia kiasi kigodo cha pesa ili kupata huduma hiyo.

Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa Bidhaa wa Netflix, Chengyi Long amesema hatua hiyo itawapa uhuru zaidi wateja wake kufurahia filamu za jukwaa hilo na watu mbalimbali kwa gharama nafuu.

“Tunatambua kuwa watu wana chaguo nyingi za burudani, kwa hivyo tunataka kuhakikisha vipengele vyovyote vipya ni rahisi na muhimu kwa wanachama, ambao usajili wao hufadhili TV na filamu zetu zote kuu,” amesema Long katika blogu ya Netflix.


Soma zaidi:


Netflix imesema itawaruhusu watu ambao tayari wanashiriki akaunti moja kuhamisha wasifu na habari na historia ya kutazama kwa akaunti ndogo ndogo.

Long amesema kampuni hiyo itasoma matumizi ya mtindo huo mpya katika nchi hizo tatu kabla ya kufanya mabadiliko popote pengine.

Mwaka jana, jukwaa hilo lilikuwa na watazamaji milioni 221.8 ambao waliongezeka kutokana na ugonjwa wa Corona ambapo watu wengi walikuwa karantini na hivyo kupata muda wa kutazama filamu. 

Hata hivyo, robo ya kwanza ya mwaka 2022, Netflix inakusudia kuongeza watumiaji milioni 2.5 tu, ongezeko ambalo jukwaa hilo limesema siyo la kuridhisha.

Huenda mpango huo mpya wa Netflix ukaisaidia kuongeza mapato yake ya kila mwaka.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV