Necta: Mitihani kidato cha nne 2025 kuanza Novemba 10

February 17, 2025 3:39 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Itaanza Novemba 10 na kutamatika Novemba 28, 2025.
  • Ni muda wa wanafunzi kufanya maandalizi ya mwisho na muhimu kuelekea mtihani.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetoa ratiba rasmi ya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2025, ambapo watahiniwa wataanza mitihani yao Novemba 10 na kuhitimisha Novemba 28, 2025. 

Mtihani wa kidato cha nne ni hatua muhimu katika safari ya elimu kwa wanafunzi ambao huashiria hitimisho la elimu ya sekondari ya kati na hutoa fursa kwa watahiniwa kuingia vyuo vya kati au kuendelea na elimu ya sekondari ya juu kwa kidato cha tano na sita.

Mtihani wa kidato cha nne ni hatua muhimu katika safari ya elimu kwa wanafunzi ambao huashiria hitimisho la elimu ya sekondari ya kati, Picha | Mtanzania.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mtihani utaanza Jumatatu ya Novemba 10, 2025 kwa somo la Uraia (Civics) ambao utaanza saa 2:00 asubuhi hadi saa tano.Mchana watahiniwa watafanya mtihani wa Biolojia (Biology 1).

Jumanne, tarehe 11 Novemba, mitihani itaendelea ambapo watahiniwa watafanya mtihani wa somo la Hesabu ( Basic Applied Mathematics 1 ) majira ya asubuhi, huku mchana  watahiniwa wakifanya mtihani wa somo la Kiswahili.

Siku ya Jumatano, Novemba 12 asubuhi, watahiniwa watafanya mtihani wa somo la Jiografia na mchana watakabiliana na mtihani wa Kingereza.

Alhamisi, Novemba 13, mitihani itaendelea na Baolojia kwa vitendo (Biology 2A Practical), huku mchana  ikiwa ni zamu ya somo la Sanaa (Fine Art 1). Na Ijumaa, tarehe 14 Novemba, watahiniwa watafanya mitihani ya Kemia 1 kwa upande wa asubuhi na Historia kwa mchana.

Wiki ya pili ya mtihani itaanza Jumatatu, Novemba 17 ambapo watahiniwa watafanya mitihani ya Fizikia 1, Sayansi ya Uhandisi, Lugha ya Kichina, Kilimo 1 na Ufundi wa Nguo na Ushonaji wa Mavazi. 

Jumanne, Novemba 18, masomo ya Kemia kwa vitendo, Fasihi ya Kingereza na Hesabu (Additional Mathematics) yatafanyika. 

Jumatano ya Novemba 19 mitihani ya Fizikia kwa Vitendo (Physics 2A Practical), (Building Construction) Uhandisi wa umeme (Electrical Engineering) na Uhandisi wa Uchoraji (Engineering Drawing) itafanyika pamoja na masomo ya biashara (Book Keeping) Ufundi wa mbao na Uchiraji na Engineering Electronics Draughting.

Alhamisi ya tarehe 20 Novemba, mitihani ya Muziki 1, Baolojia kwa vitendo (Biology 2B Practical) somo la biashara (Commerce) pamoja na masomo ya uhandisi yatafanyika. Wiki itatamatishwa kwa mitihani ya masomo ya dini (Elimu ya Biblia na Elimu ya Dini ya Kiislamu)

Mitihani mingine ya vitendo, dini, sanaa na biashara kama Sanaa (Fine Art 2) Fizikia kwa vitendo (Physics 2B Practical) Ufundi wa Nguo na Ushoonaji wa Mavazi 2 na Tehama itafanyika siku ya Jumatatu, Novemba 24.

Mitihani ya Lugha ya Kifaransa, Kemia kwa vitendo (Chemistry 2B Practical) pamoja na masomo ya uhandisi (Architectural Draughting, Electrical Draughting, Automotive Engineering) yatafanyika siku ya Jumanne, Novemba 25. 

Siku ya Jumatano, Novemba 26 watahiniwa watakabiliana na  masomo ya Muziki 2, Baolojia kwa vitendo (Biology 2C Practical)Chakula na Lishe ya Binadamu (Food and Human Nutrition) kwa asubuhi na baadae somo la elimu ya viungo (Physical Education).

Masomo ya Kemia kwa vitendo (Chemistry 2C Practical) na Tehama 2 yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 27 Novemba na mitihani itatamatika Ijumaa tarehe 28 Novemba kwa masomo ya Fizikia kwa vitendo (Physics 2C Practical) pamoja na Kilimo 2 saa sita na nusu mchana.

Umuhimu wa mtihani wa kidato cha nne

Kwa watahiniwa wengi, mtihani huu si tu fursa ya kufanikisha malengo yao ya kielimu, bali pia njia ya kujenga mustakabali wao wa maisha. kwa sababu hiyo, maandalizi thabiti ni muhimu ili kuhakikisha wanafanya vizuri.

Watahiniwa wanahimizwa kuipitia kwa umakini, kupanga ratiba zao za masomo, na kuhakikisha wanazingatia vipindi vyote vya mitihani yao. 

Wataalamu wa elimu wanashauri kuanza maandalizi mapema ikiwa imesalia takribani miezi saba kufikia mwezi Novemba kwa kutumia muda huo kwa ufanisi, kufanya mazoezi ya maswali ya mtihani wa miaka ya nyuma, na kujifunza mbinu za kusimamia muda wanapofanya mitihani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks