Nape aagiza uchunguzi vifo vya wanahabari misafara ya viongozi wa Serikali
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombolezo muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ilipofanyika shughuli ya kuaga miili ya waandishi watano waliofariki jana wakiwa kwenye ziara ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza. Picha| Mgongo Kaitira.
- Ahoji kwanini waathirika katika ajali hizo ni waandishi wa habari.
- Aagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha ripoti ya ajali zote za misafara ya viongozi zilizohusisha wanahabari.
- Serikali kuandaa itifaki kuwalinda wanahabari misafara ya viongozi wa Serikali.
Dar es Salaam/Mwanza. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha ripoti serikalini ya ajali zinazotokea kwenye misafara ya viongozi wa Serikali kuwahusisha wanahabari ili hatua zichukuliwe kuwalinda.
Waziri Nape ametoa maagizo hayo leo Januari 12, 2021 muda mfupi kabla ya kuagwa na kutoa heshima kwa waandishi wa habari watano waliofariki dunia jana katika ajali ya barabarani mkoani Simiyu.
Wanahabari hao ni sehemu ya watu 14 waliofariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace katika eneo la Nyamikoma, Wilaya ya Busega katika Mkoa wa Simiyu.
Waandishi wa habari walipoteza maisha katika ajali hiyo ni Husna Mlanzi kutoka kituo cha televisheni cha ITV, Vanny Charles (Icon), Antony Chuwa, Johari Shani (Uhuru Digital) na Abel Ngapemba ambaye ni Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mwingine ni Paulo Silanga aliyekuwa dereva ofisi ya mkuu wa mkoa aliyekuwa anaendesha gari lililobeba wanahabari siku ya ajali.
Majeneza yenye miili ya wanahabari waliofariki katika ajali ya gari jana Januari 11 inaagwa na kupewa heshima za mwisho katika uwanja wa michezo wa Nyamagana jijini Mwanza. Picha| Mwananchi.
Waziri Nape amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ajali zinazotokea katika misafara ya viongozi wa Serikali lakini waathirika wakubwa ni wanahabari, jambo ambalo linaibua maswali mengi yasiyo na majibu.
โKumekuwa na matukio ya ajali kwenye misafara mbalimbali ya viongozi wetu na bahati mbaya ajali hizi waathirika wakubwa ni wanahabari. Viongozi wenu wameguswa na jambo hili na wmaeniagiza tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara,โ amesema Nape wakati wa kuagwa kwa miili ya wanahabari hao katika viwanja vya Nyamagna mkoani Mwanza leo Januari 12.
Amesema kutokana na mfululizo wa ajali hizo, Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi na kuwasilisha ripoti serikalini ili ipitiwe na kuangalia namna ya kuweka utaratibu mzuri wa kuwalinda wanahabari wanapokuwa katika misafara ya viongozi wa Serikali.
โViongozi wangu wameniagiza kwamba wenzetu wa Jeshi la Polisi watuletee ripoti za ajali hizi tuzipitie tuone kwanini zinaguza wanahabari na tuchukue hatua ya kuweka itifaki nzuri itakayowalinda wanahabari wanapotimiza wajibu wao kwenye misafara ya viongozi wetu,โ amesema Waziri Nape na kubainisha kuwa,
โZipo sababu nyingi zinazungumzwa lakini tunataka tujilidhishe kutoka kwenye vyombo vyetu kuhakikisha kwamba tunazo sababu za kweli za kwanini sababu hizi zinawagusa zaidi wanahabari tuchukue hatua.โ
Mesema itifaki hiyo inaweza kumaliza ajali hizo kama siyo kuzipunguza kwa kiasi kikubwa.
Ajali hiyo iliyogharimu watu muhimu katika tasnia ya habari imetokea ikiwa zimezipita wiki tano tangu itokea ajali kama hiyo ilihusisha wanahabari waliokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti uliokuwa unaelekea wilayani Newala kutekeleza mradi wa mapambano ya Uviko-19.
Katika ajali hiyo iliyotokea Desemba 2, 2021, gari lililopata ajali liliwabeba John Kasembe (Azam TV), Anne Roby (D News), Adam Malima (Channel Ten) na Baraka Jamal ( Safari Redio)ย
Gari lililowabeba waandishi wa habari hao liligongana na gari lingine na kuwajeruhi wanahabari hao.ย
Soma zaidi:
-
Rais Samia atuma salamu za pole vifo vya watu 14 Simiyu
-
Wanahabari watano waliofia ajalini waagwa Mwanza
Pia ajali nyingine ilitokea Julai 3, 2020, baada ya msafara wa aliyekuwa Waziri wa Madini, Doto Biteko kupata ajali kwa kuhusisha gari lililokuwa limewabeba waandishi wa habari kukosa mwelekeo na kugonga kingo za barabara katika eneo la Murugunga, Kata ya Murusagamba, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Katika ajali hiyo, baadhi ya waandishi walipata majeraha na kupatiwa huduma ya kwanza katika Kituo cha Afya Murusagamba na kisha kupelekwa mkoani Geita kwa uchunguzi zaidi.
Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye nambari za usajili STL 3132 mali ya Wizara ya Madini iliyowabeba wanahabari Nazareth Ndekia (TBC), Emmanuel Ibrahim (Clouds), Victor Bariety ย (Chanel Ten) pamoja na Salma Mrisho (Star TV).
Pia ajali nyingine kubwa iliyogharimu maisha ya wanahabari ndani ya kipindi cha miaka sita iliyopita ni ile iliyotokea eneo la Mwika mkoani Kilimanjaro mwaka 2017 ambapo watu sita wakiwemo waandishi wa habari wawili walipoteza maisha baada ya gari lao kugongwa na gari nyingine aina ya Fuso.
Habari hii imeandikwa na wanahabari Daniel Samson (Dar es Salaam) na Mariam John (Mwanza).
Latest
