Rais Samia: Acheni kutanguliza maslahi yenu binafsi

July 26, 2024 1:55 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Akerwa na viongozi wanaotanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi ya Taifa. 
  • Aeleza kuwa viongozi wote wanapaswa kuwatii waajiri wakuu ambao ni wananchi. 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan awewataka viongozi wa Serikali kuacha kuweka mbele maslahi yao binafsi na kuwadogosha wananchi ambao ndiyo waajiri wao wakuu. 

Katika hotuba yake baada ya kuwaapisha viongozi wapya wakiwemo mawaziri aliowateua hivi karibuni, Rais Samia amesema baadhi ya viongozi wanatanguliza maslahi yao binafsi wanapopata nyazifa badala ya kuangalia maslahi mapana ya Taifa. 

 “Maslahi binafsi kama binadamu sawa lakini mbele ni maslahi ya taifa…sasa wale mliozoea kutumia nafasi zenu kujinufaisha nyinyi au kujinyanyua nyinyi kabla ya kunyanyua taifa naomba rekebisha kabla sijakuona,” amesema Rais Samia leo Julai 26, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Kauli hiyo ya Rais Samia inakuja baada ya kuwafuta kazi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye. Mwingine aliyeguswa katika panga hilo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato.


Soma zaidi: Rais Samia awafuta kazi Nape Nnauye, January Makamba


Katika hafla ya leo, Samia aliwaapisha mawaziri wanne, manaibu waziri wawili, katibu mkuu na katibu tawala mmoja baada ya kufanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri mwishoni mwa juma lililopita.

Miongoni mwa viongozi wa walioapishwa leo ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

                              

                        

Rais Samia ameeleza kuwa madaraka ni dhamana na ni sawa na nguo ya kuazima hivyo viongozi wote wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa weledi na uwajibikaji. 

“Sitarajii mwende mkadhihaki au kuwadogosha wananchi kwa sababu wao ndio sababu ya sisi kuwepo hapa kwa hiyo twendeni tukawatumikie… ,tumieni mamlaka yenu madaraka yenu kwenda kuwatumikia wananchi,” amebainisha Rais Samia katika hotuba fupi ya iliyodumu kwa takriban dakika 20. 

Katika hafla ya leo, viongozi wa juu walionekana kutuma ujumbe maalum kwa viongozi wa Serikali kuwajibika ipasavyo kazini la wanaweza kufurushwa kazini. 

Makamu wa Rais  Dk Philip Mpango amewaleza walioshiriki wa hafla hiyo kuwa hakuna kiongozi asiye na mbadala akiwemo yeye mwenyewe. 

“Asifikirie mtu kamwe kwamba ni indispensable (asiyebadilishwa) hivyo ni muhimu sana kuzingatia kama viongozi kwamba Amiri Jeshi Mkuu muda wowote anaweza kutengeneza timu yake ili kuwaletea ushindi Watanzania,” amesema Dk Mpango.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV